Jumapili, 22 Mei 2016

Sehemu ya 3, I hate you Mr.President.

RIWAYA:  I HATE YOU MR. PRESIDENT  ( 03 )

“nakupenda sana mama… wewe ndio furaha yangu pakee.” Aliongea mtoto huku akimfuta machozi mama yake.

“sitalia tena…nitakuja kulia siku utakayo oa mwanangu. Tena si kwa uchungu wa maumivu… bali kwa uchungu wa kutimiza ndoto za baba yako mlaghai.” Aliongea maneno hayo na kumkumbatia tena mtoto wake aliyemfariji kwa kumpapasa mgongoni.

“pindi tutakapokabidhiwa motto. Ni wapi tutaenda mama?”aliuliza mtotoo baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

“swali zuri mwanangu. Ila sioni haja ya kuondoka kwenye nyumba ile kwa ajili ya future yako. Unasoma kupitia mgongo wao japokua wanaitumia njia hiyo kama sababu ya kujisafisha kwa watu wasioujua ukweli wa mateso  ya nyumba hiyo.”aliongea mama yake na kumuangalia Eliyasaa.

“ ila mama, mimi sioni haja ya kuendelea kuishi kwenye nyumba ile kama wataendelea kutunyanyasa kama awali. Pia wakijribu kufanya chochote kwa mdogo wangu, basi mi nitaondoka kwenye nyumba hiyo hata kama wewe utangang;ania kubaki.” Alionea motto huyo na kulala kwenye kifua cha mama yake.

Masaa matatu baade, kila kitu kilikamilika na kupewa mtoto. Mama yake Eliyasa alikibeba kichanga na kutoka nacho nje ya hospitali. Huko nje, walimuona dereva wa mtoto wa baba mwenye nyumba akiwa nje ya hospitali hiyo.

“nimetumwa kuja kuwachukua.” Aliongea hivyo Yule dereva na wao hawakutaka hata kuhoji  kuwa ametumwa na nani. Walipanda kwenye gari hiyo na safari ya kurudi nyumbani kwao ikanzia hapo.

Walirudi nyumbani na baada ya kufika.waliingia ndani na kuwapita wenyeji wao sebuleni. Walisalamia na salamu zao zikaenda na upepo. Hakuna aliyeitikia ingawaje wali zisikia.

Hata wao hawakujali wala kusubiri kupokelewa kwa salamu zao.. waliingia chumbani kwao na kumlaza mtotoo huyo mchanga kabisa.

“eeh Mungu… naomba uwape utu japo kwa miezi kadhaa hawa watu ili malaika wako huyu asipatwe na madhara. Maana umwewapa mali lakini umewanyima ubinaadamu. Naogopa nisije nikampoteza mtoto wangu huyu mchanga kwa unyama walio nao. “

Alipiga magoti mama huyo na kuongea maneno hayo kwa sauti ndogo tu akimuambia Mungu wake juu ya usalama wa mtoto wake.

Usiku wa siku hiyo,walisikia mlango ukigongwa kwa nguvu na kuwafanya waamke.  Mama yake Eliyasaa, aliamka na kwenda kufungua bila ubishi na baba mwenye nyumba hiyo aliingia huku akiwa ameongozana na mke wake.

“yaani nyie mbwa hamna akili kabisa. Yaani wewe tumekusaidia huyu mtoto mmoja. Umeona haitoshi umeamua kutuletea na huyu mtotoo mwengine. Haya sema basi… baba wa mtotoo huyu ndio wa Eliyasaa, au hyu mtotoo nae ana baba yake mwengine?” aliongea mke wa baba mwenye ile nyumba huku akibenjua midomo yake kwa dharau.

“sina cha kukujibu Mama.. hii ni ishu binafsi sana.” Alijibu mama Eliyasa kinyonge.

“sasa kama ni ishu binafsi..utajua wewe na Mungu wako. Ila tunachokiomba kutoka kwako ni kukusanya nguo zako. Na utafute mahala pa kuipeleka familia yako kwa wazazi wenzako. Mimi sitaki wageni. Zaidi nilikua nasubiri tu uutue huo mzigo wa dhambi ulikua tumboni kwako.” Aliongea mama huyo huku akiwa ameshika noti kadhaa mkononi mwake na kumtupia usoni mama Eliyasa.

Walitoka na kuwaacha wakiwa wametaharuki. Hawakujua ni kwanini mama huyo aliyekua hana kauli nzuri siku zote, leo ameamua kuwabadilikia kiasi hicho.

Kilio kilianza upya kwa mama huyo ambaye daima hakuwahi kuyafurahia maisha ya humo ndani. Furaha yake ilikua ni kutoa machozi kwa asilimia ndogo sana kwa siku. Hali hiyo ilimfanya mpaka mtoto wake Eliyasa kumfuata na kumbembeleza.

“hakuna haja ya kulia mama. Tuondoke tu kwa usalama wa mdogo wangu. “ aliongea Eliyasa na kumtazama mdogo wake ambaye hata nuru ya macho ilikua bado hajaanza kuona.

Kiunyonge kabisa walianza kupanga nguo zao chache kwenye mabegi yao. Hawakuweza kulala zaidi ya kusubiria mapambazuko ya asubuhi ili waweze kuondoka kwenye nyumba hiyo kwa hiyari.

Mama wa mwenye nyumba hiyo hakua anatania ilie usiku wa kuamkia siku iyo alipowaambia kua hawataki, kwani alihakikisha wanatoka nje na kuufunga mlango wa chumba walichokua wana kaa.

 

Safari ilianza barabarani huku akiwa amemshika mkono Eliyasa wake huku kichanga akiwa amekishikilia kwenye mkono wake wa kushoto.

Hakua na mwamvuli wa kumkinga na jua kwa ajili ya kichanga hicho. Alichokkifanya ni kumfunika vizuri na nguo huku akili yake yote akiitumia kukilinda kichanga hicho.

Aliiongoza familia yake huku akiwa hana ramani ya ya uelekeo anaouelekea muda huo.

Masaa matatu baadae, alifika stendi ya daladala na kukaa kwenye kituo hicho huku akipata muda wa  kukinyonyesha kichanga hicho.

“naomba zile hela.” Aliongea mwanamke huko baada ya kutazama huku na huko na kuona kua kulikua na usalama maeneo waliyopo.

Baada ya kupewa. Alizihesabu na kugundua kua zilikua ni laki nne kasoro elfu ishirini.

“inabidi tutafute madalali wa huku uswahiini ili tupate chumba cha kujisitiri.” Aliongea mama huyo na kumuangalia Eliyasa.

“Sawa mama.”

Alijibu Eliyasaa na safari ya kutafuta bango la madalali lilianzia hapo.

Baada ya mwendo mfupi na kwa msaada wa watu wa karibu, waliweza kumpata dalali mmoja Maarufu na kuwapeleka kwenye nyumba moja yenye chumba cha giza.

“me papenda hapa?”

Aliuliza dalali baada ya kupewa fungua za chumba hicho na kuwaonyeshea wateja wake.

“ndio… tumeridhika ndugu yangu.”

Alijibu mama yake Eliyasa baada ya kukukagua chumba na kuridhika nacho.

Maisha yao kwa kujitegemea wenyewe yalianzia hapo huku fedha kidogo walizobakiwa nazo baada ya kulipia chumba hicho kilichowagharimu elfu ishirini kwa mwez, wakitumia kununua zuria na godoro dogo kwa ajili y kichanga hicho.

Kwa mapenzi ya Mungu na huruma yake, aliisimamia familia hii mpaka mtotoo mchanga alipotumiza miezi sita  ambapo mama huyo alilazimika kumuachisha ziwa kwa ajili ya kuwa bize katika utafutaji wa mahitaji ya hapo nymbani.

 

JAMANI, KAMA UMEIPENDA STORI HII NAOMBA SHARE KWENYE SOCIAL MEDIA ZAKO. NITAFURAHI SANA UKIFANYA HIVYO , LAKINI TAFADHARI NAOMBA USIIKOPY NA KUIBADILISHA KITU CHOCHOTE ,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni