Jumapili, 22 Mei 2016

Jini Husnat, sehemu ya 1

RIWAYA JINI HUSNAT
MTUNZI: ZUBERI MAVUGO

SEHEMU YA KWANZA.

Ulikuwa ni ukumbi mkubwa ulojaa watu wenye hela zao,kila starehe iliyopo katika dunia hii ilikwepo hapo kasino ilo lilijaa wadachi,waindi,walokuwa wakijiuza mziki mkubwa ulikuwa ukiendelea kuwaburudisha wateja wa club hiyo kulikuwa kuna walinzi wa kutosha,walokuwa tayari kupambana na kiumbe chochote kitakachotaka kuleta shida gari aina mbali mbali za kitajiri ziliingia na kutoka na wasichana warembo ni ukumbi ulosifika kwa matanuzi yote uyatakayo

JOHN VERGAN kama mwenyewe alivyopenda kujiita alikuwa counter akitupia pombe yake taratibu! machangudoa wachache walijipitisha mbele yake lakini ilo wala akulijali wengine awakuishia kujipitisha tu kwani walimfata na kutaka kutoa company lakin VERGAN hakuwa tayari,mawazo yalitawala kichwa chake aligubia bia kwa fujo aikujulikana kipi kilichomtesa kijana huyo mwenye umbo la wastani si mrefu sana wala si mfupi sana,maji ya kunde mwenye body sex mwili wa mazoezi alikuwa na kila mvuto wa kimapenzi kwa mwanamke amwangaliaye! wanawake wengi sana walimmezea mate lakin moyoni mwake alikwepo mwanamke mmoja tu MOURINE huyu ndo alomfanya VERGAN Agubie ile bia kwa hasira na hisia tele MAPENZI yalimtesa alimpenda mtu asiyempenda tena secretary wake macho yake makubwa yaliyozungukwa na nyuzi nyembamba nyeusi yalitua mkononi mwake alivaa saa ya dhahabu iliyosomeka ni saa sita na nusu usiku akashusha pumzi taratibu ni wazi alishachoka na usingizi ulishaanza kuyanyemelea macho yake kilevi kilishaanza kumlevya akajinyanyua pale huku akipepesuka na kuanza kuondo
*****
"simu unayopiga aipatikani tafadhali jaribu tena badae" ndiyo kauli ilojibu upande wa pili JOHN VERGAN alizidi kunywa bia yake taratibu mpaka alipotosheka kwa vyovyote muda ule MOURINE asingeweza kuja akiwa anapepesuka taratibu alinyanyuka na kuelekea nje kwa hatua fupi aliiendea gari yake ilokuwa nje na kujipakia ndani toka jioni alikwepo katika hoteli ile mpaka muda ule aliiwasha gari na kuiondoa kwa kasi.
-.....-.....-.....-
MOURINE msichana mrembo kiumbo na secretary wake VERGAN akiwa ndani ya gari yake jioni hii moyoni mwake alikuwa na raha sana! kitendo cha BOSI wake kumuitaji hotelini kilimpa faraja,ni kweli alimpenda bosi wake yule.na bosi wake alishamwonesha ishara zote za kumpenda,akutaka kumkubali kwa kutopenda kuonekana mrahisi ila siku hii ya leo alijihisi hali flan si ya kawaida alijihisi KUMPENDA na kuitaji kuwa pamoja naye kimapenzi hisia zile zikamfanya aongeze mwendo wa gari lake kumuwai mwanaume yule ghafla akiwa katika mwendo mkali akakatisha mwanamke mrembo mbele ya gari.MOURINE akajaribu kupiga break ila gari likamvaa dada yule MOURINE akiwa kachanganyikiwa baada ya kujiisi kumgonga mdada akashuka kwa speed mpaka mbele ya gari lake AKUKUWA NA MAITI WALA MDADA MOURINE akashtuka,kwa haraka akarudi garini na kujaribu kuwasha gari GARI LIKAGOMA,akazidi kuchanganyikiwa.akashika simu yake nayo kwa ajabu ikawa imezima charg.safari ya MOURINE ikawa imefia hapo.

BADO JOHN VERGAN moyo wake ulijaa simanzi ghafla akiwa kwenye mwendo wa wastani mbele yake akamuona msichana mrembo,msichana alozivuta na kuziamisha HISIA zake akazidi kupunguza mwendo wa gari na alipo mfikia dada yule kabla ajamsemesha dada yule akamuwahi
"kaka naomba lifti" VERGAN akujibu swali lile kwani akili yake ilikuwa katika umbo zuri la mrembo yule! umbo namba nane,mwenye asili ya kiindi akika alikuwa na mvuto wa ajabu.
"mimi naita JOHN mwenzangu sijui unaitwa nani?" dada yule ndani ya gari alikaribishwa na swali
"MIMI NAITWA HUSNAT".....,.

Macho ya VERGAN yalikuwa katika mapaja mazuri yalokuwa muda wazi wakati huo,binti yule aliyejitambulisha kama HUSNAT alivaa kimini kidogo kilicho acha mapaja yake wazi! kutokana na msukumo wa pombe VERGAN alijikuta akishindwa kuzuia HISIA zake nzito kwa dada yule! akamtongoza! dada yule akuwa na kizuizi VERGAN akimchukulia kama changudoa akaelekea katika nyumba yake.akiwa na mwanamke yule ndani akipania kulala naye usiku mzima LAITI ANGEJUA?
-......-.....-.....-
Ilikuwa ni nyumba kubwa na ya kifahari gari aliyepanda VERGAN na msichana mrembo HUSNAT iliingia mpaka parking VERGAN akiwa kamshika mkono JINI yule wakatoka na kuelekea sebuleni ambapo awakukaa sana wakaelekea chumbani wakapanda kitandani kila mmoja akionekana kumuitaji mwenzake! VERGAN katu akuziona kwato zilizokuwa katika miguu ya bibie yule,macho yake ya kungaa katika giza pia kwa macho yake ya kawaida aliyaona kawaida! wakazama penzini! penzi ambalo katu VERGAN akuwai kulipata kwa binadamu wa kawaida,penzi liliyomlevya na kumpa usingizi mzito.baada ya VERGAN kulala jini HUSNAT akuwa na muda wa kupoteza akavaa nguo zake zote akanyoosha mkono wake juu barua ikatokea akaiweka pale kitandani na GHAFLA AKATOWEKA.

VERGAN alipapasa mbele yake apakuwa na mtu,akafumbua macho yake taratibu kajua cha asubuh kalitokeza kutarifu sasa kumepambazuka,VERGAN alishtuka na kucheki mlango
"UKUFUNGULIWA" Akakumbuka juu ya kukutana na HUSNA jana
"au nilikuwa naota?! hapana!" bado VERGAN alikuwa katika hali za sintofahamu akakurupuka kitandani pale akiita kwa nguvu kama mweu
"HUSNA! HUSNA! HUSNA!" Bado hakukuwa na jibu! akaingia chooni,bafuni ndani kwa ndani bado akukuwa na mtu!.vergan akiwa kama kachanganyikiwa akafungua mlango na kutoka nje alipomkuta kitatu
"umemuona msichana katoka humu ndani asubuhi hii?"
"msichana? msichana yupi bosi?"
"yule nlokuja naye jana usiku!"........

*****

JOHN VERGAN akazidi kuchanganyikiwa!,akaenda sebuleni akajitupa somani!,mawazo yakaanza kupishana kama mishale ya saa "uyu binti atakuwa kaenda wapi yarabi?! mbona mlango ukufunguliwa? mlinzi naye anasema sikuingia na mtu jana usiku au nilikuwa naota? hapana hapana hapana nilimpa binti lifti HUSNA alinambia anaitwa HUSNA nikampenda! nkamchukua nkaja naye akanipa penzi tamu ambalo sijawai kulipata alafu! alafu ikawaje? HUSNA! HUSNA! hapana si ndoto kuna kitu" alijiuliza VERGAN na kujijibu mwenyewe akajinyanyua na kurudi tena chumbani macho yakadondokea kitandani kilikuwa shaghala baghala kuonesha kwamba usiku kucha kilitumika kikazidi kumpa picha sahihi kwa kile akiwazacho macho yake yakatua mezani akakuta barua imefungwa vizuri huku mkono ukiwa unatetemeka akaifata na kuishika ilinukia harufu nzuri,harufu ya manukato,alikumbuka manukato hayo ni ya HUSNA akaichukua ile barua na kuifungua na kuanza kuisoma naaam macho yalimtoka pima

"DEAR SAMAHANI! KWA KUONDOKA BILA KUKUTA HARIFU NILIHITAJIKA HARAKA NYUMBANI NA WAZAZI ASUBUHI NJEMA WAKO KIPENZI HUSNA NTARUDI"

VERGAN akashangaa,ilikuwa lazima ashangae
"aliitajika nyumbani!?,alipitia wapi?! aliondoka saa ngapi?!!" bado maswali mfululizo yalizidi kumuandama akairudia tena kuisoma ile barua yenye hati nzuri ila akupata majibu aloyaitaji akaikunja barua yake na kuirudisha pale mezani alitoka akaenda kuoga,kuswaki,kuvaa nguo za kazini dakika chache zilizofatia zilimkuta mezani akinywa chai aloandaliwa na mfanyakazi wake JASMINI alipomaliza alinyanyuka na kuliendea gari lake akapanda na kuelelea kazini.alimpita secretary wake MOURINE bila salamu na kuingia ofisini kwake MOURINE akaingia ili kumuuliza kama aliitaji amletee chai tofauti na matarajio yake VERGAN akaanza kushusha lawama
"hivi MOURINE kwa nini unantesa hivi? kwa nini jana ulindanganya na ukuja? kama ulikuwa utaki si ungenambia?.........
**
***
MOURINE huku akiwa anatetemeka akamwangalia bosi wake! "hapana bosi niliaribikiwa na gari"
"comon MOURINE kwa nini ukunambia kwa simu nikajua?"
"simu nayo iliisha chaji bosi...." wakati wakiendelea kuongea ghafla simu ya VERGAN ikaita alipoangalia kwenye scrini ilisomeka HUSNAT.Ubongo wake ukatingishika! akampa ishara MOURINE aondoke maswali yakaanza kutiririka katika kichwa chake!
"nani kampa namba zangu?" aliwaza alikuwa na uhakika akumpa wala akuserv namba zake.ili kupata jibu akaamua kuipokea
"alooo!" VERGAN alisema
"vipi sweet za kazi" sauti nyororo kama kinanda iliuliza VERGAN akaipuuza Na kwa hasira akamuuliza
"nani kakupa namba zangu?"
"si wewe sweet umenipa jana?"
"mimi sijakupa namba zangu"
"umenipa beby"
"sijakupa"
"umenipa!"
"ok ulikuwa unasemaje?" VERGAN aliuliza kwa hasira
"nilikuwa naitaji tuonane" HUSNA alisihi
"siwezi kuonana na wewe" VERGAN alijibu kwa jeuri akapokewa na kicheko kitamu kisha sauti laini ikafatia (basi my love ntakuja hapo kazini jioni tuondoke wote!) hapo hapo akakata simu ubongo wa VERGAN kwa mara nyingine ukatingishika idadi ya maswali yasiyo na majibu yakatiririka! (uyu ni binadamu au jini?,anapafahamu hapa kazini?) bila kujielewa akaanza kusarch namba ya HUSNA kusudi azipige NO AZIKWEPO!!! hakuweza kujizuia kutetemeka kwenye recevd azikwepo.wakati akiwa katika mawazo ya sintofahamu ghafla meseji ikaingia katika simu yake (usiwaze sana dear utaumwa na kichwa) namba zilikuwa ni jina tu JINA BILA NAMBA? akazipiga zikakataa! moyo ukaanza kumwenda mbio akaishika simu ya mezani na kumpigia secretary wake MOURINE naomba mwambie ZUBERI namwitaji ofisini kwangu dakika chache badae ZUBER aliingia akamwonesha ishara aketi.alikuwa ni kijana mrefu,alikuwa ndo meneja baada ya yeye ZUBER ndo alikuwa chini yake alimwamini kijana yule alikuwa ndo mshauri wake,siri zake ZUBERI alizijua,siri za ZUBER naye alizijua walikuwa kama ndugu waloshibana..

VERGAN alimweleza ZUBERI kila kitu!,"dah pole bosi huyo atakuwa ni jini tu! kubali ukatae! kwanza embu nioneshe hizo msg zake! mahana siamin" VERGAN akatii na kuchomoa simu yake mfukoni akaanza kutafuta zile meseji inbox HAZIKWEPO na anakumbuka akuzifuta kabisa! bumbuwazi likauvaa uso wake
"kah meseji azipo kak!"
"nini?" ZUBER akaoji kwa mshangao
"sijazifuta lakini nashangaa kutoziona!"
"basi BOSI jibu ndo ilo huyo atakuwa ni jini mahaba!"
"sasa nfanyeje rafiki yangu?"
"kuna mtaalamu namfahamu ntakupeleka"
"hapana best mim ni msomi siamini hao watu wengi wao matapeli....."
Katika vitu ambavyo JOHN VERGAN akuvipenda ni kuamini ushirikina "mganga wa kienyeji!" ZUBER alijaribu kumbembeleza lakin VERGAN akuwa tayari,mwisho akakata na tamaa!
"ina maana uyu ni mtu au jini?" bado maswali yasiyo na majibu yaliambaa katika kichwa chake.
"sura ya HUSNAT ikamjia kichwani mwake wakati walivyokuwa wakifanya mapenzi" miguno ya kimapenzi na hata sura yake alivyoikunja,utamu alokuwa nao,HISIA zikampanda,tabasamu likamponyoka.
"atakuwa ni binadamu anacheza na akili yangu tu!" akajifariji upendo moyon mwake ukafumuka kama mvua za masika ALIANZA KUMPENDA!. Akashangaa kumpenda ghafla kiasi icho! moyo wake aliujua vyema.aukuwa wa mtu aliyeyapendekeza mapenz akupenda kujiumiza kichwa kama kwa MOURINE aliyepanga kumuoa,lakini MOURINE anamzingua,alipobahatika kumuona HUSNA akajua jibu lake limepatikana lakini vitabia tabia vyake vinamshangaza naye ni jini? aoe jini?
"no siwezi kumpenda HUSNA!" akapingana kwa nguvu na HISIA zake
ilipofika jioni wakati anajiandaa kuondoka ghafla mlango ukafunguliwa na HUSNAT akaingia na tabasamu pana usoni uzuri wake ulikuwa mara mbili ya mwanzo bumbuwazi likauvaa uso wa VERGA akutegemea kama angekuja kweli mbona secretary wake ajampgia simu? alijawa na khofu ulochanganyikana na woga ilikuwa lazima aogope alikuwa kavaa gauni jekundu refu lililo mkaa vyema.akaenda kuketi kwenye viti vya wageni na kumpa mkono VERGA....

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni