Jumatano, 25 Mei 2016

Mwanza Kupokea Tani 500 Za Sukari

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema mkoa wa Mwanza unategemea kupokea Tani 500 za Sukari zitakazo ingia katika mkoa huu zikitokea kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar tarehe 24, Mei, 2016, ambazo zinaingizwa mkoani hapo na muagizaji na Msambazaji P.H  Shah.

Hata hivyo mkuu wa mkoa ameonya watu watakao uza sukari hiyo kinyume na bei elekezi kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja nakufikishwa katika vyombo vya dola.

Mongella amesema pia kwamba, kupitia kamati yakushughulikia sukari, tayari wametoa maelekezo kwa Wakuu wa wilaya jinsi yakushughulikia suala la sukari na kwamba wasambazaji wote katika Wilaya lazima wazingatie maelekezo bila kuvunja utaratibu utakao wekwa.

Mahitaji ya sukari katika mkoa wa Mwanza ni Tani 1,500 kwa wiki kwa matumizi ya kawaida kwa wananchi wake, hivyo kuwasili kwa tani 500 itasaidia kupunguza uhaba wa sukari  unao ukabili  mkoa huu kwa sasa..

Hata hivyo mkuu wa mkoa amewatoa wanachi hofu juu ya sukari kwakusema, tayari viwanda vya hapa nchini vimekwisha anza uzalishaji wa sukari na kwamba muda si mrefu tatizo la sukari litapungua kama sio kuisha kabisa.

Imetolewa na Atley J. Kuni
Afisa habari na Mahusiano, Ofisi ya mkuu wa Mkoa
MWANZA -24, Mei 2016

Viongozi Wa Africa Wataka Mahusiano Yaboreshwe Kwa Maendeleo Ya Bara

WAKUU wa nchi za Afrika wametaka kuwepo na juhudi za pamoja katika kukabiliana na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabiachi yanayolikumba bara hilo.

Kauli hiyo ilitolewa jana mchana (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati wa majadiliano baina ya viongozi kutoka Zambia, Chad, Nigeria, Msumbiji na Tanzania mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 51 wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano cha kimataifa wa Mulungushi, jijini Lusaka, Zambia.

Wakishiriki kwenye mjadala wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliohusu Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi, viongozi hao walisema bara la Afrika linahitaji kupata maendeleo zaidi licha ya tatizo la nishati linalolikumba bara hilo hivi sasa.

Akichangia mjadala huo, Rais wa Zambia, Bw. Edgar Lungu alisema nchi yake imepania kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme vijijini lakini imekuwa ikikabiliwa na tatizo la uhaba wa mvua kwa zaidi ya miaka miwili hali ambayo alisema imechangia kukosekana kwa umeme katika maeneo mengi nchini humo.

“Uhaba wa mvua umepunguza kiwango cha maji katika bwawa la Kariba ambalo hutumika kuzalisha umeme nchini mwetu. Na hapa kwetu, karibu asilimia 80 ya umeme wetu, unategemea uzalishaji wa umeme kutokana na vyanzo vya maji,”  alisema.

Rais wa Chad, Bw. Idriss Deby Itno aliitaka benki ya AfDB ichukue nafasi ya mdau mkuu kwenye uwekezaji wa sekta ya nishati na kuzisadia nchi za bara hili kupata mitaji ya uwekezaji na ushauri wa kitaalamu.

“Tunahitaji kutumia fursa ambazo benki yetu inazo katika kukabilianana changamato za ukosefu wa nishati. Tukiweza kutekeleza jambo hilo, tutafanikiwa kuwa na miradi ambayo ni makini na kwa maana hiyo tutaweza kuliangaza bara letu la Afrika kwa kupata mwanga wa uhakika,” alisema.

Kwa upande wake, Makamiu wa Rais wa Nigeria, Prof, Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika halina budi budi kuweka kipaumbele kwenye masuala ya maendeleo yake wakati likitafuta suluhisho la kukabiliana na athari za mazingira.

“Tunapaswa kutafuta njia za kubalance mahitaji makubwa ya umeme ambayo bara letu linakabiliwa nayo dhidi ya athari za kimazingira ambazo zinapigiwa kelele na mataifa makuna na zinahatarisha kutunyima fursa ya kuendelea haraka kama ilivyokuwa kwao,” alisema na kuongeza:

“Kama nchi zilizoendelea zinataka sana kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi, zinatakiwa zitupatie fedha, teknolojia na wataalamu ambao watasaidia kuendesha mitambo ili tupate nishati safi kutokana na mafuta ya petroli na dizeli sababu ni rasilmali ambazo tunazo.”

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema ili kuondokana na tatizo la nishati, kuna haja ya kuwa na viongozi wenye utashi wa kisiasa ambao watakuwa tayari kuruhusu uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya nishati na kuongeza kuwa Tanzania inapitia upya sheria zake ili kuruhusu miradi mikubwa ya uwekezaji kwenye sekta hiyo.

Aliwaambia washiriki wa mkutano huo kwamba milango ya uwekezaji Tanzania iko wazi kwa ajili ya wawekezaji walio tayari kuwekeza kwenye sekta hiyo na kutaja fursa ambazo Tanzania inazo kwenye sekta ya nishati ikiwemo gesi asilia, makaa ya mawe, madini ya urani, maji, upepo na nishati ya joto kutoka ardhini (geothermal energy).

Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário alisema kuna haja ya kuwa na taasisi ya uzalishaji na ugawaji umeme ya pamoja (electricity pool) ambayo itaruhusu wazalishaji wa umeme wawauzie wanunuzi wakubwa.

Waziri Mkuu ambaye yuko Lusaka kuhudhuria mkutano huo wa ADB kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, amerejea nchini leo (Jumatano, Mei 25, 2016).

Dk Shein Amuwakilisha JPM Comoro

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein anaondoka leo jioni kwenda Muungano wa Visiwa vya Comoro kwa ziara ya siku mbili.

Akiwa nchini humo Dk Shein atamuwakilisha Rais Dk John Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo, Azali Assoumani Boinakher.

Kuapishwa kwa Boinakher kunafuatia ushindi wake alioupata katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika tarehe 10 Aprili 2016 na ule wa marudio katika kisiwa cha Anjouan uliofanyika tarehe 11 Mei, 2016.

Sherehe hizo za kuapishwa Rais huyo mteule zitafanyika kesho katika kiwanja cha Mpira cha mjini Moroni na zinatarajiwa kuhudhuriwa  na viongozi mbalimbali kutoka nje ya nchi hiyo.

Katika ziara hiyo Dk Shein amefuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Bora , Issa Haji Ussi Gavu na Mshauri wa Rais Uhusiano wa Kimataifa, Uchumi na Uwekezaji Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa.

Makampuni 52 Yajitokeza Kuwekeza Sekta Ya Umeme Bongo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi sasa Serikali imekwishapokea maombi 52 kutoka makampuni mbalimbali ambayo yanataka kuwekeza kwenye sekta ya umeme nchini Tanzania.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati akizungumza na Watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Lusaka, Zambia.

“Haya maombi yamekwishapokelewa na wenye makampuni wamekwishahojiwa kuangalia uwezo walionao katika suala zima la uwekezaji wanaotaka kuufanya, na tukiwapata wenye uwezo na wenye nia ya dhati watapatiwa miradi ya kuiendesha,” alisema.

Aliwataka Watanzania hao waishio Zambia watumie fursa ya uwepo wao huko kutafuta marafiki ambao wanaweza kuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali nchini kwani Serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu wakati wananchi wanahitaji kupatiwa huduma muhimu.

“Serikali peke yake haiwezi kufanya kazi ya uwekezaji kwa hiyo tunahitaji kushirikiana na sekta binafsi, taasisi za kifedha na washirika wa maendeleo na ndiyo maana kule kwenye mkutano nimewaeleza washiriki kwamba milango ya uwekezaji Tanzania iko wazi."

Alisema kupatikana kwa umeme wa uhakika kutawezesha wananchi wengi zaidi kujiingiza katika shughuli za kiuchumi na hivyo kuinua uchumi wa nchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Alisema malengo ya Serikali ya awamu ya tano ni kuona kuwa nchi inakuwa na mitambo mingi ya kuzalisha umeme na umeme wote unaozalishwa na mitambo hiyo inaunganishwa na gridi ya Taifa ili kuondokana na tatizo la mgao wa umeme nchini.

Alisema Tanzania ina vyanzo vingi vya nishati vikiwemo gesi asilia, makaa ya mawe, madini ya urani, maji, upepo, nishati ya joto kutoka ardhini (geothermal energy) na nishati inayotokana na vinyesi vya mifugo (biomass) ambayo alisema vinatumika kwa watu wachache (siyo kitaifa).

Alisema kupatikana kwa gesi asilia nchini kumeleta neema ambapo mabomba ya gesi yamekwishajengwa kutoka Mtwara hadi Kinyerezi na kutoka Kilwa-Songosongo hadi Dar es Salaam. 

“Sasa hivi kuna utafiti unaendelea juu ya uwezekano wa kusambaza gesi ya kupikia majumbani. Tumeanza pale Mikocheni (DSM) na sasa hivi wanafanya utafiti mwingine kule Mtwara ili wananchi waweze kutumia gesi hii kupikia badala ya mkaa,” alisema.

Akielezea kuhusu uwekezaji kwenye makaa ya mawe, Waziri Mkuu alisema Serikali imelenga kutumia makaa ya mawe ili kuendeshea mitambo ya kwenye viwanda vikubwa badala ya kutumia umeme au mafuta ya dizeli kama inavyofanyika sasa.

 “Baadhi ya wenye viwanda wanabadilisha mifumo ya kuendeshea mashine zao ili iweze kuendana na teknolojia ya makaa ya mawe pindi tu uchimbaji ukishika kasi,” alisema.

Akifafanua kuhusu juhudi za Serikali katika kusambaza nishati ya umeme, Waziri Mkuu alisema tangu kuanzishwa kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), vijiji zaidi ya 3,000 katika ya vijiji 12,000 vilivyopo nchini vimefikiwa na nishati ya umeme.

“Tulianza na REA awamu ya kwanza, awamu ya pili na sasa tunaenda awamu ya tatu. Hata mkipiga simu kwa ndugu zenu vijijini, mtakuta katika kila kata kuna vijiji kati ya vinne hadi vitano ambavyo vimefikiwa na nishati ya umeme kupitia mradi wa REA,” alisema.

Waziri Mkuu amerejea nchini leo (Jumatano, Mei 25, 2016).

Jumapili, 22 Mei 2016

Tuhuma za Ubadhirifu wa Sh bilioni 1.4 za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana Zatua TAKUKURU


TUHUMA za ubadhirifu wa Sh bilioni 1.4 za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana, zilizotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa Halmashauri ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma, zimefikishwa kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Senyi Ngaga, alisema Takukuru inakamilisha uchunguzi wa kina ili wahusika waliofanya ubadhirifu huo wachukuliwe hatua za kisheria. 

Alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Alisema upo ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi uliofanywa na wahusika waliopewa dhamana ya kusimamia matumizi yake. 

Ngaga alisema, ofisi yake baada ya kuunda tume ndogo na kubaini hilo, uchunguzi wa awali unaonesha Sh milioni 513 zimefanyiwa ubadhirifu .

Alisema, aliona ni vyema achukue hatua ya kukabidhi tuhuma hizo kwa Takukuru wafanye uchunguzi wa kina kutambua ni nani aliyehusika na ubadhirifu huo.

 Alisema, taarifa na majina ya wahusika waliofanya hivyo itatolewa baadaye Takukuru ikikamilisha kazi yake.

“Takukuru inaendelea na uchunguzi, ikikamilisha taarifa itatolewa. Katika maelezo yangu ya awali kwenye Baraza la Madiwani lililokaa juzi sikuhukumu mtu wala kusema amehusika, hivyo tusubiri tutajulishwa,” alisema.

Aliongeza kuwa, uchunguzi huo utakapokamilika, taarifa husika zitapelekwa kwa Mwenyekiti wa Baraza la Ulinzi na Usalama mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu awasilishe kwa Waziri mwenye dhamana.

Awali, tuhuma za ubadhirifu huo, zilitolewa na Mkuu wa Wilaya kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa wilaya hiyo, Mei 11, mwaka huu.

Familia Yasema Kifo cha Wilson Kabwe Hakikutokana na Mshtuko wa Kufukuzwa Kazi na Rais Magufuli


Familia ya Wilson Kabwe, aliyekuwa mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, imesema ndugu yao alishawatoa wasiwasi kuhusu tuhuma zilizosababisha kusimamishwa kazi na Rais John Magufuli na kwamba alitamani uchunguzi ufanyike haraka ili ukweli ujulikane. 

Kabwe aliyefariki dunia Mei 20 kwa ugonjwa wa saratani ya tezi dume jijini Dar es Salaam, alisimamishwa kazi na Rais Magufuli wakati wa uzinduzi wa daraja la Mwalimu Nyerere lililopo Kigamboni Aprili 19. 

Miongoni mwa makosa yaliyosababisha kusimamishwa kwake ni madai ya kusaini mkataba kwa kutumia sheria ndogo ya mwaka 2004 kutoza magari yanayotoka kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo (UBT) Sh4000 na mwingine wa Sh8,000 chini ya sheria ndogo mwaka 2009. 

Kulikuwa pia na madai ya kukithiri kwa rushwa katika kituo hicho hasa katika kutoa magari na ukodishwaji wa vyumba vya kupangisha, kinyume na utaratibu na kuongeza muda wa mzabuni aliyeingia mkataba na jiji wa maegesho ya magari. 

Akizungumza jana nyumbani kwao, Masaki jijini Dar es Salaam, mtoto wa marehemu, Joseph Kabwe alisema kifo cha baba yao hakikutokana na mshtuko wa kusimamishwa kazi, bali alianza kuugua muda mrefu na alishawaambia kuwa hana wasiwasi na tuhuma hizo, bali anataka uchunguzi ufanyike haraka. 

“Alikuwa na saratani ya tezi dume na alikuwa akitumia dawa za chemotherapy ambazo ni kali sana na zilisababisha kuathirika kwa ini. Hata siku baba anatumbuliwa pale darajani alisema hana wasiwasi kwa sababu kila kitu kiko sawa sawa,” alisema Joseph. 

“Baba alitutaka tusiwe na wasiwasi, tena mwenyewe alikuwa akisisitiza kuwa anatamani matokeo ya uchunguzi yatoke mapema ili ukweli ujulikane,” alisema. 

Jana msibani kulikuwa na viongozi tofauti wa ngazi ya mkoa waliofika kutoa pole. Kaimu mkurugenzi wa jiji aliyekuwapo msibani hapo, Sarah Yohana alisema Halmashauri ya Jiji inashiriki msiba huo kwa kuwa Kabwe alikuwa mtumishi wao. 

“Yule alikuwa mtumishi wa halmahsauri na ana haki zake kama mtumishi mwingine yoyote. Tutatoa jeneza, gari la kusafirishia maiti, chakula na rambirambi,” alisema Sarah. 

Sarah alisema alikabidhiwa ofisi na Kabwe tangu Novemba mwaka jana baada ya kwenda kutibiwa nchini India. Kuhusu taratibu za utumishi, alisema licha ya Rais kumsimamisha kazi, hawakuwahi kuona barua yoyote iliyoletwa inayohusu kusimamishwa kwake. 

“Inawezekana alipewa kwa njia nyingine, lakini sisi hatukuona barua ya kusimamishwa. Yule ni ‘presidential appointee’ (mteule wa Rais), yeye ndiye mwenye mamlaka na watu wake wa kufanya uchunguzi. Sisi hatujui, inawezekana wanafanya uchunguzi wao huko wenyewe,” alisema Sarah. 

Jana Msemaji wa familia hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Eliab Mkenga Kabwe alisema hawana ugomvi wowote na Serikali huku akimkana mtu aliyejitambulisha kuwa msemaji wa familia hiyo, Dk. Zawadi Machuve aliyetoa maelezo kwa waandishi wa habari juzi kuwa hawataki viongozi wa Serikali wakanyage msibani. 

Aliongeza kuwa familia hiyo inatambua na kuthamini mchango wa Serikali katika kugharamia matibabu na huduma zote za mazishi. 

Alisema Makonda aliyetoa tuhuma za Kabwe kabla ya Rais Magufuli kutangaza kumsimamisha kazi, anatarajiwa kufika msibani hapo muda wowote. 

“Mkuu wa Mkoa, Makonda bado hajafika hapa, lakini anaweza kufika wakati wowote. Unajua yeye ndiye mwenye mkoa wake kwa hiyo atafika tu wakati wowote,” alisema.

Mbali na viongozi wa jiji waliokuwapo kwenye msiba huo, viongozi wa mikoa mingine akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo na mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga walikuwapo msibani hapo. 

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, ambaye alikuwapo eneo hilo, ameshauri msiba huo uhamishiwe katika ukumbi wa Karimjee ikiwa ni kumpa heshima Kabwe aliyekuwa kiongozi wa jiji, lakini hakuna dalili za kufanya hivyo.

CCM: Hatutamuadhibu Kitwanga Mara Mbili


CCM imesema kitendo cha Rais John Magufuli kumvua uwaziri Charles Kitwanga kutokana na kuingia bungeni akiwa amelewa, kimedhihirisha kuwa bado kuna baadhi ya watumishi wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma, lakini hakitachukua hatua kwa kuwa ameshaadhibiwa.

Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka jana  alisema kitendo cha Kitwanga kuingia bungeni akiwa amelewa kimewapa fundisho na sasa wanajua kuwa kuna baadhi ya watumishi waliopewa dhamana na chama hicho, lakini wanakiuka miiko ya maadili ya utumishi wa umma, jambo ambalo ni kinyume na taratibu zao.

Sendeka alisema licha ya kwamba Rais Magufuli amechukua hatua juu ya hilo na kutoa adhabu, CCM itaendelea kufuatilia kwa ukaribu mienendo ya wanasiasa waliopewa dhamana na chama hicho.

“Hatutasita kuchukua hatua endapo tutabaini kuna kada anayekiuka maadili ya viongozi wa umma,” alisema Sendeka.

Alisema CCM inampongeza Rais Magufuli kwa uamuzi aliochukua dhidi ya Kitwanga kwa kuwa hatua hiyo imedhihirisha kauli aliyowahi kusema kwamba hataangalia mtu usoni wala kujali kabila au dini, ikiwa mtu huyo atakiuka miiko ya uongozi.

Kuhusu CCM kumuadhibu Kitwanga, Sendeka alisema adhabu aliyopewa na Rais inatosha. “Hukumu haitolewi mara mbili,” alisema Sendeka.

Kitwanga ambaye anatajwa kwenye sakata la utekelezaji mbovu wa mkataba wa kufunga vifaa vya kuchukua alama za vidole baina ya Jeshi la Polisi na kampuni ya Lugumi Enterprises, alivuliwa ukuu wa wizara hiyo nyeti baada ya kutinga ndani ya ukumbi wa Bunge Ijumaa asubuhi na kujibu maswali akiwa amelewa.

Hadi jana jioni, Rais Magufuli alikuwa bado hajajaza nafasi hiyo nyeti huku wananchi wakibashiri jina la mrithi wa Kitwanga kwa kuangalia jinsi marais waliopita walivyokuwa wakijaza nafasi kama wa kumpandisha naibu waziri wa wizara hiyo au nyingine, kumteua mtu anayemfahamu, kubadilisha mawaziri na kumrejesha aliyewahi kuwa waziri ama kuteua kutoka kwenye kanda anayotoka aliyetimuliwa.

Mara nyingi katika uteuzi wa mawaziri, viongozi wakuu wa nchi wamekuwa na utaratibu wa kuwapandisha baadhi ya manaibu kuwa mawaziri, kuwapa uwaziri wabunge ambao amewateua au kuteua waziri kutoka katika mkoa ambao anatokea waziri aliyeondolewa.

Mara zote saba ambazo Rais mstaafu Jakaya Kikwete alifanya mabadiliko ya baraza la mawaziri alifuata utaratibu huo.

Alipomuondoa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ambaye ni mbunge kutoka mkoa Kagera alimteua mbunge mwingine kutoka mkoa huo, Charles Mwijage kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini.Kwa sasa Mwijage ni Waziri wa Viwanda na Biashara. 

Utaratibu huo unaweza kunufaisha wabunge sita wa majimbo yaliyopo mkoa wa Mwanza ambao ni Chalres Tizeba (Buchosa), Mansoor Hirani (Kwimba), Kiswaga Boniventura (Magu), Stanslaus Mabula (Nyamagana), William Ngeleja (Sengerema) na Richard Ndassa (Sumve).

Mbali na Kitwanga ambaye aliteuliwa kuwa waziri kutoka mkoa huo, Rais pia alimteua mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Iwapo Rais atatumia utaratibu wa kupandisha naibu waziri kuwa waziri, neema huenda ikamuangukia mbunge wa Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandishi Hamad Masauni au naibu mawaziri kutoka wizara nyingine. Katiba pia inampa Rais fursa ya kuteua wabunge 10 na tayari ameshatumia nafasi sita.

Chadema Wamtaka Rais Magufuli Amfuate Lowassa Ili Amshauri Kuhusu Swala la Sukari


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtaka Rais John Magufuli kuweka siasa kando na kuomba ushauri kwa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ili kutatua tatizo la kuadimika kwa sukari.

Kauli hiyo ilitolewa na naibu katibu mkuu wa Chadema, Salim Mwalimu juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Moto wilayani Monduli Mkoa wa Arusha ambako Lowassa alizungumza na wananchi kuwashukuru kwa kumpigia kura na akatangaza mpango wa kuzunguka nchi nzima kwa lengo hilo.

Tangu Rais atangaze kudhibiti uagizaji sukari kutoka nje na baadaye Bodi ya Sukari kutangaza bei elekezi, bidhaa hiyo muhimu imepanda bei kutoka Sh1,800 hadi kufikia Sh5,000 kwa kilo na kwa sasa imeadimika madukani, wakati Serikali ikisaka wafanyabiashara inaowatuhumu kuwa wameificha kwenye maghala kwa lengo la kuihujumu.

Akizungumza kabla ya kumruhusu Lowassa kuongea na wananchi hao, Mwalimu alisema inaonekana tatizo la sukari linaelekea kuishinda Serikali na hivyo inahitaji msaada wa ushauri.

“Tatizo la sukari kalianzisha yeye mwenyewe Magufuli na sasa anashindwa kulitatua,” alisema Mwalimu na kuongeza:

“Mtu pekee atakayemsaidia ni Lowassa. Huyu alijipanga na alijiandaa kuongoza nchi.”

Mwalimu alisema Lowassa amevumilia mengi kwa kuwa amenyanyaswa, ameonewa na kusimangwa lakini hakujibu.

“Amepitia kipimo cha mwisho cha utu, ni cha mwisho. Walimuonea mchana kweupe akavumilia. Walimsimanga mchana kweupe mpaka watoto wadogo walikuwa wakimuona Lowassa kama vile saizi yao, akavumilia,” alisema Mwalimu.

“Ninajua vijana waliumia, mzee. Lakini leo warudi nyuma wafikirie maisha yao. Ni nani angetoka nyumbani kwa kauli moja ya Lowassa, kumshika mtoto wake mkono kumpeleka shule kama Lowassa angeangalia ushetani na kumuacha Mungu,” alisema akirejea kauli ya Lowassa kuwa alikuwa akipigiwa simu na watu kumtaka atoe kauli baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana kutangazwa, lakini akaawaambia watulie.

Lowassa, ambaye aligombea urais kwa tiketi ya Chadema baada ya kuenguliwa CCM, alishika nafasi ya pili kwenye mbio hizo akipata kura milioni 6.07 idadi ambayo ni rekodi kwa mgombea wa upinzani tangu siasa za ushindani zirejeshwe mwaka 1992. Magufuli aliibuka mshindi kwa kupata kura milioni 8.8.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Lowassa aliwataka wananchi kuendelea kutulia, akisema mwaka 2020 hauko mbali na Chadema inaendelea kujipanga upya ili kuhakikisha inashika dola na kuondoa kero zao.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa Chadema kutoka makao makuu, mkoa pamoja na makada waliojiunga wakitokea CCM wa wilaya ya Monduli, Lowassa alisema wafuasi wa ukawa wajiandae kwa mikutano hiyo.

Huku akishangiliwa na wananchi hao waliokuwa wakimkatisha kwa kelele za shangwe, Lowassa alisema kwa kushirikiana na viongozi wenzake wamejipanga kufanya ziara ya kuijenga Chadema nchi nzima.

“Nina hakika tumewashika pabaya CCM na tumewaumiza sana. Sasa kwa kushirikiana na viongozi wenzangu tutazunguka nchi nzima tunataka kuiweka Chadema kwenye chama cha siasa na si uanaharakati,” alisema.

Akizungumzia Uchaguzi Mkuu uliomalizika Oktoba 25 mwaka jana, Lowassa aliwashukuru wananchi kwa kumpa kura nyingi akisema hata walioiba kura zake wanajua na dunia inajua kuwa alishinda.

“Niliamua kukaa kimya kwani najua ningesema jambo moja nchi yetu ingeangamia. Na vijana kila kona ya nchi walikuwa wakinipigia simu wakidai wanasubiri neno kutoka kwangu,” alisema.

“Sikufurahishwa na kwenda Ikulu kwa mikono iliyojaa damu. Kuna siku nitakwenda Ikulu kwa mikono safi ya Watanzania, nina hakika na rafiki zetu wanajua kabisa kwamba hawakushinda.”

TANZANITE ONE yamjia juu mbunge James Ole Millya....Yamtuhumu Kupotosha Bunge na Umma Bila Kufanya Utafiti.

KAMPUNI ya Sky Group Associates inayomiliki mgodi wa tanzanite wa TanzaniteOne, imesema Mbunge wa Simanjiro, James ole Millya amepotosha Bunge na umma juu ya suala zima la ununuzi wa hisa kwa kampuni hiyo.

Akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini mwishoni mwa wiki, Millya alisema Sky Group Associates iliyonunua hisa kwa Kampuni ya TanzaniteOne na kumiliki kitalu C Mirerani wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, haikufuata taratibu za ununuzi wa hisa hizo na kuwatuhumu baadhi ya mawaziri kuwa walihusika katika kupindisha taratibu.

Aliwataja mawaziri hao kuwa ni George Simbachawene na Jenista Mhagama, ambaye hata hivyo alikanusha madai hayo ; na ametaka taratibu za Kibunge zimlamzishe Millya, kukanusha au kuthibitisha madai yake. 

Mbali ya hilo, mbunge huyo aliituhumu kampuni hiyo kwa kuwafukuza kazi wafanyakazi 201, bila ya kufuata utaratibu na kwamba inawanyanyasa .

Akizungumza na mwandishi wetu, Mwanasheria wa kampuni hiyo, Kisaka Mnzava alisema uongozi umesikitishwa na kauli ya Millya, kwa kusema alitoa kauli bila kufanya utafiti wa kina. 

Mnzava alimtaka mbunge huyo, kujiridhisha kwa kufanya utafiti wa kina namna hisa za TanzaniteOne zilivyouzwa kwa Sky Group, inayomilikiwa na wazawa kwa asilimia 100.

Alisema wamiliki wa hisa wanajulikana na kama anahitaji kuwafahamu, anapaswa kwenda Mamlaka ya Usajili wa Leseni za Kampuni (Brela) kujiridhisha. 

Alisema hakuna waziri wala kiongozi yeyote mwingine wa serikali, anayemiliki hisa katika Sky Group Associates.

Alisema kampuni imeshalipa kodi yote ya serikali, na kampuni hiyo sio ya mfukoni, kama anavyodai mbunge huyo. 

Mnzava alisema shughuli za uzalishaji zinasimamiwa kikamilifu kati ya Sky Group na serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (Stamico), ambao ni wabia wa mgodi huo, na kwamba hakuna madini yanayoibwa kama mbunge huyo alivyosema.

Alisema hakuna njia ya mkato, iliyofanywa katika ununuzi wa hisa ; na hakuna waziri yeyote aliyehusika katika kusaidia kupindisha taratibu, kwani kila kitu kipo wazi. 

Alisema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu), Jenista Mhagama hana ndugu na mtu anayefanya kazi TanzaniteOne.

Akizungumzia kufukuzwa kwa wafanyakazi 201, mwanasheria huyo alisema waliofukuzwa kazi ni wafanyakazi hatari kwa mustakabali wa kampuni, kwani ni wachochezi na wenye hila za kutaka kuihujumu kampuni hiyo ili ilete maafa. 

Alisema kugoma ni kosa kisheria na kama mgomo haukufuata taratibu, sheria lazima zichukue taratibu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya May 23

Watumishi hewa waziponza Bank Dar-es-salaaam, Zapewa Barua Kurejesha Mabilioni ya Fedha, Makonda ahamua kulalanazo Mbere...

Watumishi hewa waziponza Bank Dar-es-salaaam, Zapewa Barua Kurejesha Mabilioni ya Fedha, Makonda ahamua kulalanazo Mbere...

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku 21 kwa benki zilizokuwa zikitumika kuweka mishahara ya watumishi hewa, kurejesha fedha hizo serikalini ; au kubainisha waliokuwa wakitumia akaunti hizo, kuchukua fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Makonda alisema benki ndio pekee wanaoweza kusaidia mkoa, kutambua wahusika waliokuwa wanatumia akaunti hizo pamoja na wale waliokuwa wanachukua fedha hizo.

Alisema watu hao wasipopatikana, inamaanisha fedha bado zipo katika benki hizo, hivyo zinapaswa kuzirudisha serikalini zifanye maendeleo kwa wananchi. 

“Tayari tumeshaziandikia benki hizo barua na kuwapatia majina na akaunti na kuwataka kutuwasilishia majina ya wahusika, waliohusika na akaunti hizo ili kusaidia kutambua mtandao mzima wa wahusika wa suala la watumishi hewa ambao wameigharimu serikali,” alisema Makonda.

Alitaja benki hizo pamoja na fedha wanazodai kuwa ni benki ya NMB ambayo inadaiwa zaidi ya Sh bilioni mbili, CRDB zaidi ya milioni 400, NBC zaidi ya milioni 141, DCB milioni 85, Standard Chartered zaidi ya Sh milioni mbili na Community Benki zaidi ya milioni 100.

“Hakuna mtu anayeweza kutumia akaunti ya mtu bila kufuata taratibu za kibenki, hata kama mtu amefariki kuna taratibu za kufuata ndipo apate akaunti, naamini benki hizi zitasaidia kuwatambua wahusika wote,” alisisitiza.

Aidha, alizitaka benki hizo kufunga huduma za akaunti hizo ;na zisifanye malipo yoyote mpaka fedha hizo zitakapopatikana. 

Mpaka sasa, Mkoa wa Dar es Salaam umebainika kuwa na watumishi hewa 283, ambao wanadaiwa kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 3.6 ambazo zilitumika kuwalipa mishahara.

Familia ya Marehemu Kabwe: Hatujakataa kuishirikisha Serikali

Familia ya Marehemu Kabwe: Hatujakataa kuishirikisha Serikali

Waziri Nape Nnauye akimpongeza Wema Sepetu wakati wa uzinduzi wa Wema Mobile Application.


Waziri Nape Nnauye akitoa neno na pongezi wakati wa uzinduzi wa Wema Mobile Application


 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akimpa mkono wa pongezi msanii wa filamu hapa nchini,Wema Sepetu kwa kubuni huduma ya kisasa kabisa WEMA MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar 

 Mwanadada Wema Sepetu akifafanua jambo kwa  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye kabla ya uzinduzi wa huduma hiyo kufanyika mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar. 

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akizungumza kabla ya kuzindua mfumo wa kisasa kabisa wa msanii wa filamu hapa nchini,WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION mbele ya waandishi wa habari,katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar
 Msanii mahiri wa filamu hapa nchini Maadam Wema Sepetu akizunguma mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),jioni  ya leo katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar kabla ya kuzindua huduma yake WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION,ambayo itakuwa ikijumuisa matukio yake yote sambamba na video mbalimbali  yatakayowekwa kwenye mfumo wa teknolojia ya kisasa kupitia simu za mikononi.

Wema Sepetu amesema kuwa huu ni mwanzo mzuri na anaahidi kutumia huduma hiyo kutoa elimu kunufaisha jamii,kutangaza sanaa na utamaduni wetu,kuwa karibu na wapenzi ama mashabiki wake wote watakaokuwa wanahitaji kupata habari zake za kweli na uhakika.

Mfumo huo wa kipekee kabisa kwa mwanadada huyo,umezinduliwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye,mfumo ambao utaweza kumuunganisha Wema na jamii Duniani kote."Mfumo wangu huu ni wa kipekee na wa kwanza katika Afrika Mashariki kwa msanii wa tasnia ya Filamu,mfumo huu utaleta fursa nyingi sana zikiwemo ajira kwa vijana na wasanii wenzangu na kutambulika kirahisi"alisema Wema Sepetu.

Kujua mafanikio na Umuhimu wa kazi za Usanii Tanzania,huduma ya Wema Sepetu Mobile ni rahisi na ya uhakika,unatuma neno WEMA kwenda 15404,tayari unakuwa umeishajiunga na utaanza kupokea taarifa na habari za Wema sepetu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno,picha na video kutegemeana na aina ya simu yako unayotumia.

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh,Nape Nnauye akimpongeza mwanadada Wema Sepetu kwa kubuni mfumo ambao utaweza kumuunganisha Wema na jamii Duniani kote na pia utamsaidia kumuingizia kipato na kuweza kuisaidia jamii inayomzunguka kwa namna moja ama nyingine.

Mtaalamu wa huduma za mitandao kutoka Push Mobile,Haji Yussuph akifafanua jambo kuhusiana na huduma hiyo ya WEMA SEPETU MOBILE APPLICATION

 Meneja wa Biashara  wa Hartmann Trader ambao ndio watoa huduma ya Wema Sepetu Mobile Application,Cecil Mhina akifafanua namna huduma hiyo inavyoweza kutumika na pia maelezo kadhaa namna ya kujinga na kupata taarifa mbalimbali na video kupitia huduma hiyo

 Mmoja wa wageni waalikwa akiuliza swali kwa Wema Sepetu namna huduma hiyo inavyoweza kufanya kazi.

Lowassa Kuanza Rasmi Mikutano Ya Kuimarisha Chama Nchi Nzima

Lowassa Kuanza Mikutano Ya Kuimarisha Chama Nchi Nzima

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeneo (CHADEMA) na aliyekuwa Mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu uliopita kwa tiketi ya chama hicho na kuungwa mkono na UKAWA, Edward Lowassa akisalimiana na viongozi wa walemavu wilayani Monduli kwenye Mkutano wa kwanza wa kuimarisha chama nchi nzima. 

BAKWATA WALAANI VIKALI MAUWAJI YA WATATU MWANZA.

Bakwata walaani vikali mauwaji ya watatu mwanza.

Wakati  Rais John Magufuli akitoa salamu za pole kwa wakazi wa jiji la Mwanza, kutokana na mauaji ya watu watatu waliouawa kwa kukatwa mapanga wakiwa msikitini, Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) limelaani mauaji hayo.

Aidha, Baraza hilo limewataka waislamu kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili wahalifu hao waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Kauli hiyo imetolewa na Mufti na Shehe Mkuu Abubakari Zubeir wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mauaji hayo yaliyotokea Jumatano saa mbili usiku wakati waumini hao wakifanya ibada. 

Shehe Zubeir alisema tukio hilo la watu wasiojulikana kuvamia na kuwaua waumini msikitini ni la kinyama ambalo halipaswi kuvumiliwa.

“Kwa niaba ya Bakwata tunalaani vikali tukio hili pamoja na kuwataka waislamu kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu. Lakini pia nawaomba Waislamu na wananchi kwa ujumla kuvipa ushirikiano vyombo vyetu vya usalama ili wahalifu hawa wapatikane,” alisema Shehe Zubeir.

Alisema Uislamu ni dini ambayo moja ya misingi yake ni kulinda nafasi kama anavyosema Mwenyezi Mungu katika Kitabu Kitakatifu cha Quran na kuongeza baraza hilo linawapa pole wafiwa wote pamoja na waumini wa Masjid Rahmaan kwa msiba huo.

Aidha, alitoa agizo kwa Bakwata Mkoa wa Mwanza kufuatilia kwa karibu hali za majeruhi na wafiwa.

“Kama ambavyo naawagiza Bakwata Mkoa wa Mwanza nawaomba pia taasisi mbalimbali za Kiislamu pamoja na Waislamu na Watanzania kwa ujumla kuwa tayari katika kusaidia familia za wafiwa kwani wanahitaji kufarijiwa na kusaidiwa,” alisema.

Sehemu ya 3, I hate you Mr.President.

RIWAYA:  I HATE YOU MR. PRESIDENT  ( 03 )

“nakupenda sana mama… wewe ndio furaha yangu pakee.” Aliongea mtoto huku akimfuta machozi mama yake.

“sitalia tena…nitakuja kulia siku utakayo oa mwanangu. Tena si kwa uchungu wa maumivu… bali kwa uchungu wa kutimiza ndoto za baba yako mlaghai.” Aliongea maneno hayo na kumkumbatia tena mtoto wake aliyemfariji kwa kumpapasa mgongoni.

“pindi tutakapokabidhiwa motto. Ni wapi tutaenda mama?”aliuliza mtotoo baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

“swali zuri mwanangu. Ila sioni haja ya kuondoka kwenye nyumba ile kwa ajili ya future yako. Unasoma kupitia mgongo wao japokua wanaitumia njia hiyo kama sababu ya kujisafisha kwa watu wasioujua ukweli wa mateso  ya nyumba hiyo.”aliongea mama yake na kumuangalia Eliyasaa.

“ ila mama, mimi sioni haja ya kuendelea kuishi kwenye nyumba ile kama wataendelea kutunyanyasa kama awali. Pia wakijribu kufanya chochote kwa mdogo wangu, basi mi nitaondoka kwenye nyumba hiyo hata kama wewe utangang;ania kubaki.” Alionea motto huyo na kulala kwenye kifua cha mama yake.

Masaa matatu baade, kila kitu kilikamilika na kupewa mtoto. Mama yake Eliyasa alikibeba kichanga na kutoka nacho nje ya hospitali. Huko nje, walimuona dereva wa mtoto wa baba mwenye nyumba akiwa nje ya hospitali hiyo.

“nimetumwa kuja kuwachukua.” Aliongea hivyo Yule dereva na wao hawakutaka hata kuhoji  kuwa ametumwa na nani. Walipanda kwenye gari hiyo na safari ya kurudi nyumbani kwao ikanzia hapo.

Walirudi nyumbani na baada ya kufika.waliingia ndani na kuwapita wenyeji wao sebuleni. Walisalamia na salamu zao zikaenda na upepo. Hakuna aliyeitikia ingawaje wali zisikia.

Hata wao hawakujali wala kusubiri kupokelewa kwa salamu zao.. waliingia chumbani kwao na kumlaza mtotoo huyo mchanga kabisa.

“eeh Mungu… naomba uwape utu japo kwa miezi kadhaa hawa watu ili malaika wako huyu asipatwe na madhara. Maana umwewapa mali lakini umewanyima ubinaadamu. Naogopa nisije nikampoteza mtoto wangu huyu mchanga kwa unyama walio nao. “

Alipiga magoti mama huyo na kuongea maneno hayo kwa sauti ndogo tu akimuambia Mungu wake juu ya usalama wa mtoto wake.

Usiku wa siku hiyo,walisikia mlango ukigongwa kwa nguvu na kuwafanya waamke.  Mama yake Eliyasaa, aliamka na kwenda kufungua bila ubishi na baba mwenye nyumba hiyo aliingia huku akiwa ameongozana na mke wake.

“yaani nyie mbwa hamna akili kabisa. Yaani wewe tumekusaidia huyu mtoto mmoja. Umeona haitoshi umeamua kutuletea na huyu mtotoo mwengine. Haya sema basi… baba wa mtotoo huyu ndio wa Eliyasaa, au hyu mtotoo nae ana baba yake mwengine?” aliongea mke wa baba mwenye ile nyumba huku akibenjua midomo yake kwa dharau.

“sina cha kukujibu Mama.. hii ni ishu binafsi sana.” Alijibu mama Eliyasa kinyonge.

“sasa kama ni ishu binafsi..utajua wewe na Mungu wako. Ila tunachokiomba kutoka kwako ni kukusanya nguo zako. Na utafute mahala pa kuipeleka familia yako kwa wazazi wenzako. Mimi sitaki wageni. Zaidi nilikua nasubiri tu uutue huo mzigo wa dhambi ulikua tumboni kwako.” Aliongea mama huyo huku akiwa ameshika noti kadhaa mkononi mwake na kumtupia usoni mama Eliyasa.

Walitoka na kuwaacha wakiwa wametaharuki. Hawakujua ni kwanini mama huyo aliyekua hana kauli nzuri siku zote, leo ameamua kuwabadilikia kiasi hicho.

Kilio kilianza upya kwa mama huyo ambaye daima hakuwahi kuyafurahia maisha ya humo ndani. Furaha yake ilikua ni kutoa machozi kwa asilimia ndogo sana kwa siku. Hali hiyo ilimfanya mpaka mtoto wake Eliyasa kumfuata na kumbembeleza.

“hakuna haja ya kulia mama. Tuondoke tu kwa usalama wa mdogo wangu. “ aliongea Eliyasa na kumtazama mdogo wake ambaye hata nuru ya macho ilikua bado hajaanza kuona.

Kiunyonge kabisa walianza kupanga nguo zao chache kwenye mabegi yao. Hawakuweza kulala zaidi ya kusubiria mapambazuko ya asubuhi ili waweze kuondoka kwenye nyumba hiyo kwa hiyari.

Mama wa mwenye nyumba hiyo hakua anatania ilie usiku wa kuamkia siku iyo alipowaambia kua hawataki, kwani alihakikisha wanatoka nje na kuufunga mlango wa chumba walichokua wana kaa.

 

Safari ilianza barabarani huku akiwa amemshika mkono Eliyasa wake huku kichanga akiwa amekishikilia kwenye mkono wake wa kushoto.

Hakua na mwamvuli wa kumkinga na jua kwa ajili ya kichanga hicho. Alichokkifanya ni kumfunika vizuri na nguo huku akili yake yote akiitumia kukilinda kichanga hicho.

Aliiongoza familia yake huku akiwa hana ramani ya ya uelekeo anaouelekea muda huo.

Masaa matatu baadae, alifika stendi ya daladala na kukaa kwenye kituo hicho huku akipata muda wa  kukinyonyesha kichanga hicho.

“naomba zile hela.” Aliongea mwanamke huko baada ya kutazama huku na huko na kuona kua kulikua na usalama maeneo waliyopo.

Baada ya kupewa. Alizihesabu na kugundua kua zilikua ni laki nne kasoro elfu ishirini.

“inabidi tutafute madalali wa huku uswahiini ili tupate chumba cha kujisitiri.” Aliongea mama huyo na kumuangalia Eliyasa.

“Sawa mama.”

Alijibu Eliyasaa na safari ya kutafuta bango la madalali lilianzia hapo.

Baada ya mwendo mfupi na kwa msaada wa watu wa karibu, waliweza kumpata dalali mmoja Maarufu na kuwapeleka kwenye nyumba moja yenye chumba cha giza.

“me papenda hapa?”

Aliuliza dalali baada ya kupewa fungua za chumba hicho na kuwaonyeshea wateja wake.

“ndio… tumeridhika ndugu yangu.”

Alijibu mama yake Eliyasa baada ya kukukagua chumba na kuridhika nacho.

Maisha yao kwa kujitegemea wenyewe yalianzia hapo huku fedha kidogo walizobakiwa nazo baada ya kulipia chumba hicho kilichowagharimu elfu ishirini kwa mwez, wakitumia kununua zuria na godoro dogo kwa ajili y kichanga hicho.

Kwa mapenzi ya Mungu na huruma yake, aliisimamia familia hii mpaka mtotoo mchanga alipotumiza miezi sita  ambapo mama huyo alilazimika kumuachisha ziwa kwa ajili ya kuwa bize katika utafutaji wa mahitaji ya hapo nymbani.

 

JAMANI, KAMA UMEIPENDA STORI HII NAOMBA SHARE KWENYE SOCIAL MEDIA ZAKO. NITAFURAHI SANA UKIFANYA HIVYO , LAKINI TAFADHARI NAOMBA USIIKOPY NA KUIBADILISHA KITU CHOCHOTE ,

I hate you Mr.President, sehemu ya 1&2.

RIWAYA:  I HATE YOU MR. PRESIDENT  ( 01 & 02 )

 
Mtawanyiko wa mawingu mekundu ndio ulioibadilishwa taswira ya mchana na kuwa usiku baada ya dakaki kadhaa kupita. Taa mbali mbali ziliwashwa kuashiria kua msaada wa jua haukuwepo tena na mwanga wa mwezi ulipo juu hautoshi kulifanya anga kuwa na nuru ya kutosha.

Sauti ya mwanamke aliaye kua akilia kwa uchungu ilisikika kwenye chumba chake huku hakuna mtu mwengine aliyekua anazijali zaidi ya mtoto wake pakee aliyekua pembeni yake akilia huku akihangaika bila kujua ni kitu gani kilichompata mama yake.

“tumbooo…. Naumiaaaaa… Mungu nisaidiee…nisaidie mimiiiiii”

Aliendelea kulia mwanamke huyo ambaye  huku aki hangaika na tumbo lake kubwa lililoonekana kuwa na ujauzito usiopungua miezi Tisa.

“Baba…. Baba….”

Aliita Yule mtoto baada ya kwenda kugonga kwenye chumba cha pili kwa muda mrefu bila mafanikio. Alifanya hivyo mara kadhaa kila aliporudi na kumkuta mama yake akiwa kwenye hali mbaya kama hiyo.

Kilio hicho kilichoambatana na uchungu mkubwa au patao mwanamke huyo, ndio uliomfanya ajaribu kutambaa angalau atoke nje.

“mama…. Tuliaa.. utapona.”

Aliendelea kuongea Yule mtoto mdogo huku akilia na yeye kwa uchungu kwa jinsi alivyokua anamuona mama yake anavyoteseka kwa maumivu ayapatayo.

Chumba cha tatu alikaa mtoto mdogo wa mwenye nyumba hiyo. Aliamka na baada ya kusikia sauti za watu hao waliokua wakilia huku yule mtoto akim bembeleza mama yake.

 Aliamka Yule mtoto wa chumba kingine  na kwenda  kwenye chumba hicho na kumsaidia kupiga simu kwenye hospital moja ya karibu na muda mfupi baadae gari ya kubebea wagonjwa ilifika kwenye nyumba hiyo.

Kwa kushirikiana na mlinzi wa getini. Waliweza kumbeba mgonjwa huyo na kumpandisha kwenye kitanda  maalumu na kumpandisha kwenye gari hiyo tayari kwa kumuwahisha hospitalini.

Alipofika huko alipokelewa haraka na kuwahishwa kwenye chumba maalumu kilichopo kwenye ward ya wazazi.

“Eliyasa…. Tulia. Usiwe na wasi. Mama  yako atapona tu.” Aliongea Yule mtoto wa kike aliyewasaidia baada ya Yule mtoto ELIYASA kuambiwa asubiri nje kwa muda usiojulikana.

Eliyasaa alijiinamia huku akiwa na mawazo mengi sana kuhusuiana na hali aliyokua nayo mama yake. Japokua alikua ni mtoto mdogo mwenye umri wa miaka saba tu, lakini alielewa kila kitu kutokana na maisha aliyoyapitia toka siku aliyoletwa duniani.

Simu ya Yule mtoto wa kike iliita na alipoangalia kwenye kioo cha simu yake. Jina la Lovely daddy lilitokea na kumfanya mtoto huyo asimame.

“baba ananihitaji, nitarudi tena kesho.”

Aliongea huyo msichana bila kuipokea simu ya baba yake na kuondoka zake na kumuacha Eliyasa akiwa amejiinamia huku akilia kiume. Hakutoa sauti ila machozi pekee yalidhihirisha maumivu aliyokua nayo juu ya maisha ya mama yake.

                                         *****************************

Baada ya Yule mtoto kufika nyumbani kwao. Alimkuta baba yake akiwa kwenye mlango wa kuingilia sebuleni usiku huo huku akiwa amekunja sura . hakuwahi kukasirika mbele yake kama alivvyokasirika siku hiyo.

“hivi YASINTA, niongee na nini ili uelewe kua unahitajika kuwa mbali na ile familia?.... sasa kilichokupeleka huko ni nini?” aliongea baba yake kwa ukali.

“hicho ndicho kilichokufanya ukasirike baba. Wale ni viumbe na Mungu katuumba na roho za kuhurumiana sisi kwa sisi. Bila kujali kua wao hawana thamnani kama yetu hapa duniani.lakini kwa Mungu tuna thamani sawa baba.”  Aliongea Yule mtoto mdogo mwenye umri wa miaka Tisa.

“hivi unataka tuwahurumie kwa kiwango gani. Hivi unafikiri nikiwa fukuza nyumbani kwangu watapata wapi hifadhi wale. Halafu jitu linafanya umalaya wakati anasaidiwa tu hapa. Wewe ungemuacha ajifungue hapa kwa shida ndio siku nyingine angeacha umalaya wake na kuzuia mimba nyingine. Sasa nakupa onya la mwisho… sihitaji kukuona ukiwa kariribu na familia ile. Sihitaji …sihitaji. Nimerudia mara zote hilo ili kukuonyesha ni jinsi gani nilivyokataa swala la wewe kushirikiana nao. Na kama utakiuka na kuwa nao. Utawaponza.”

Aliongea baba yake na kurudi chumbani kwake kwa hasira.

“kwanini baba anakua na roho ya kikatii kiasi hiki kwa viumbe hawa wa Mungu. Hata kama wamekosa. Angewasamehe tu.”

Aliongea peke yake huku kichwa chake kikiwa bado hakijaafikiana na baba yake juu ya kuwaacha watu hao wanaishi nyumba moja lakini maisha yao yakiwa yana utofaut mkubwa.

                                               ****************************

Juhudi za madaktari katika kuokoa maisha ya mama yake Eliyasa zilizidi kugonga mwamba baada ya kugundua kua anapoteza kiwango kikubwa cha damu.

“hata Benk yetu ya damu nayo imeishiwa… tufanyeje Dokta.” Aliongea mmoja wa manesi aliyekua anamuwekea damu mama yake Elyasa.

“hatuna budi… muite ndugu yake na tuongee nae atafute damu kwa ajili ya maisha ya mtu wao. Wakati sisi tunaendelea na utafiti wa mimba yake ikiwemo kumuwekea maji ya uchungu ili ajifungue haraka.” Alishauri dokta na nesi akatoka haraka na kumkuta Yule dogo akiwa amejiinamia.

“mtoto…kuna ndugu yenu mwengine mkubwa zaidi yako ambaye tunaweza kumpata kwa muda huu?” aliuliza Nesi baada yakumshtua Eliyasa.

“mimi ndio ndugu yake pekee ambaye naweza sema kua natakiwa kujua chochote kuhusu mgonjwa wangu.” Aliongea mtoto huyo kijasiri na kumfanya mpaka nesi kumshangaa kwa jinsi alivyonyoosha maelezo.

“nifuate.”

Aliongea nesi maneno hayo na Eliyasa bila kusubiri alianza kumfuata na kuingia nae kwenye chumba alicholazwa mama yake na kumuona akiwa macho lakini akiwa na dripu mbili za damu zikiingia mwilini kwake kwa pamoja.

“mama yako anahitaji damu nyingi sana ili tuokoe maisha yake. Na sisi uwezo wetu ni chupa nne za damu. Tumepungukiwa na chupa tatu. Sasa unatakiwa hivi sasa tukupime ili tujue kama unaweza kumtolea damu mama yako japo chupa moja. Na baadae upate msaada kwa wasamaria wema ili tuweze kumsaidia.”

Aliongea Daktari baada ya kuhakikisha kua hakuna mtu mwengine anayeweza kufanya hivyo zaidi ya mtoto huyo aliyejitambulisha kuwa huyo mgonjwa ni mama yake.

“nipo tayari mtoe hata hizo chupa tatu kama zitawezekana.. ninachokihitaji ni uhai wa mama yangu na mdogo wangu aliyekuwepo Tumboni.”

Aliongea mtoto huyo kwa sauti iliyojaa uchungu huku akimuangalia mama yake ambaye hakuweza kuongea kitu zaidi ya kutoa machozi tu huku akiona ni jinsi gani mtoto wake alivyojibebesha msalaba mzito kuliko umri wake.

Daktari alimchukua na kwenda kumpima japo kua alikua anajua kua umri wa mtoto huyo haujafikia hatua ya kutoa damu. Ila kwakua hakuna aliyekua na damu group O kwa wakati huo, waliamini kua huyo mtoto anaweza kuwa na damu itakayoweza kusaidia kuokoa maisha ya mama yake.

“oooh shiiiit”

Ulikua mguno wa daktari baada ya kugundua kua damu ya mtoto huyo ilikua haiendani na damu ya mama yake.

“inatakiwa uandike bango au kwenda kuomba watu wenye damu group O huko unapokwenda. Maana bila kufanya hivyo maisha ya mama yako yapo hatarini.”

Alishauri Daktari baada ya kumpa ukweli Yule mtoto. Bila kuaga, aliingia uswahilini na kuokota boksi kubwa aliloliandika kwa maandishi makubwa kwa maker pen.

“kila mwenye uchungu na mama yake. Basi anisaidie damu ya kumuokoa mama yangu. Kama una damu group O, basi ndio muokozi wa maisha ya mama yangu na mlezi wangu pekee.”

Bango hilo alilikamata  na kupita nalo mitaani. Lilikua na ujumbe mzito sana uliogusa watu wengi waliojitokeza na kumuuliza kwa nini aliamua kuandika vile.

Nusu saa baadae, madaktari walishangaa kuona kundi la watu wapatao hamsini wakiongozana na Yule mtoto wakiwa tayari kutoa damu.

Tabasamu la daktari lilimpa mtuamaini mtoto huyo kua kuna uwezekano maisha ya mama yake na mdogo wake aliyekua tumboni yanaweza yakaendelea na kifo kika kaa mbali nao.

Idadi hiyo ya watu iliisaidia hata benki ya hospitali hiyo iliyofilisika damu ya group O kuongezeka kwa kasi kutokana na motto huyo.

Kila dakika isogeayo, ndio hatua za uwezekano wa kumrudisha mama yake katika haliya kawaida inavyozidi kuendelea vizuri.hatimaye yale maji ya uchungu waliyomuwekea yalifanya kazi na kusababisha aanze kulalamika na baadae kujifungua kwa njia ya kawaida.

“hongera. Umefanikiwa kokoa maisha ya mama yako na mdogo wako wa kiume.”

Aliongea Daktari na kumsababishia mtoto huyo kulia machozi ya furaha.

“kweli dokta?” aliuliza tena ili apate uhakika wa kile alichokisikia.

“kweli.. wewe ni mtoto jasiri sana. Nakutabiria makubwa sana kwenye maisha yako.” Aliongea Daktari na kuonyesha wazi kua alikua amefurahia uwepo wa mtoto huyo maeneo hayo.

“naweza kumuona?” aliuliza baada ya kuwa na hamu ya kumuona mama yake.

“unaweza kumuona. Yupo vizuri kabisa.”

Aliruhusu daktari na mtoto huyo alibisha hodi kwenye chumba cha mama yake.

“karibu muokozi wangu”

Aliitikia mama yake baada ya kuisikia sauti ya Eliyasa. Alikua anaijua kama tebo ya pili. Kila mara alipenda kuwa karibu na mwanaye huyo.

Alifika mtoto huyo huku michirizi ya machozi ikiwa katika mashavu yake. Hakuamini kua ni kweli aliyeitoa sauti yake kumkaribisha ni mama yake. Roho ilimuuma sana baada ya kuona dripu ya damu ikiendelea kuingia katika mwili wa mama yake.

“wewe ni shujaa wa dunia yangu, sijui vitu nilivyotendewa na wazazi wangu toka na zaliwa. Ila hiki ulichokitenda mwanangu ni zaidi ya mtu yeyote aliyewahi kutenda kitu kizito kama hiki atika maisha yangu. Nakupenda sana mwanangu. Daima nayasahau machungu ya baba yako kila nikuonapo. Haujawahi kunikosea. Ila hata mimi sijakosea kukuzaa wewe. Ila aliyenipa mimba ndio mwenye makosa ya kukufanya uishi kwa tabu bila sababu kiumbe wa Mungu.”

Alilalamika mama huku machozi yanamtoka na kumfanya mtoto huyo kuzidi kulia kwa kwikwi.

“usiyamalize machozi yako mwanangu wakati nipo hai. Siku nikifa utalia nini?... acha machungu ya dunia yapite, nina imani faraja ipo mbele yetu. Tusichoke kusubiri. Bila kujali itachukua muda gani kuifikia.” Aliongeza mama yake na kumfuta machozi mtoto wake aliyekua kasimama pembeni ya kitanda.

“ila kwanini mama hauwi mkweli katika mambo yako na kila siku unaamua kunificha. Hata kama umri wangu bado. Ila unatakiwa usinifiche kila kitu kinachonihusu. Kimfano, mpaka hivi sasa bado hujanipa jibu sahihi kuhusiana na baba yangu… kwanini?”aliuliza mtoto kwa uchungu. Si kwa mapenzi ya baba yake, ila kwa kuchukia kuona mama yake akipata tabu peke yake wakati baba yake yupo hai.

“sio kwamba sitaki kuku eleza mwanangu. Ila muda bado hujafika. Ila nakuahidi kua. Pindi utakapo timiza miaka kumi. Basi nitakuambia kila kitu kuhusiana na maisha yangu.” Aliongea mama yake na kumshika kichwani mtoto wake huyo aliyekua mtiifu kuliko utiifu wenyewe.

“nimekuelewa mama. Ila kama ingetokea bahati mbaya umepoteza maisha, unafikiri ni nani angeweza kuni dadavulia siri uliyoiweka mchagoni mwa moyo wako?,. kumbuka mama. Mimi sihitaji kwenda kwa baba yangu hata siku moja. Ila kumjua ni jambo zuri. Au unaona nina kukosea nikimuulizia?” aliuliza mttoto swali lililomfanya mama yake atoe tena machozi.

“nakuomba mwanangu usinikumbushe machungu ya nyuma kabla sijaamua kukuelezea mwenye we kwa ridhaa yangu. Nakuomba badilisha mada hiyo mwanangu.” Aliongea mama huyo huku machozi yanamtoka. Hapo ndipo Yule mtoto alipojiona mkosaji na kuamua kutumia shati lake na kumfuta mama yake machozi.

“nisamehe mama, sio kusudio langu kukuliza mama yangu. Sitakuuliza tena mama…. Nyamaza kulia mama. Siku ya harusi yangu utalia nini?”

Aliongea Yule mtoto huku machozi yanamtoka . Maneno ya harusi yangu utalia lini, yalimfanya mama yake ajitahidi kunyanyuka na kumkumbatia.

Anayakumbuka sana hayo maneno matamu aliyoambiwa na mwanaume aliyebadilisha maisha yake kipindi ambapo alikua msichana mbichi kabisa tena akiwa bado hajalijua jiji vizuri. Sasa hivi amepitia hatua mbaya ambazo anaamini hakuna mtu ambaye angeweza kuvumilia kama angezipia hatua hizo.

Moyo ulimuuma na kumuangalia motto wake mdogo sana huku akimfuta machozi yaliyokua yakitiriririka bila kikomo kwenye mashavu yake.

“nakupenda sana mama… wewe ndio furaha yangu pakee.” Aliongea mtoto huku akimfuta machozi mama yake.

“sitalia tena…nitakuja kulia siku utakayooa mwanangu. Tena si kwa uchungu wa maumivu… bali kwa uchungu wa kutimiza ndoto za baba yako mlaghai.” Aliongea maneno hayo na kumkumbatia tena motto wake aliyemfariji kwa kumpapasa mgongoni.

ITAENDELEA ………………

TAFADHARI NAOMBA USIIKOPY NA KUIBADILISHA KITU CHOCHOTE

Wema Haoni Ndani kabisaaa Kwa Gigy Money!

Wema Haoni Ndani Kwa Gigy Money! Ni Moto Balaaa..

Ndani ya muda mfupi wa ustaa wake ambao hauna hata nusu mwaka, muuza nyago (video queen) ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amegeuka habari baada ya kudaiwa kuwa mtungo au msururu wake wa wanaume mastaa, unatishia kuvunja rekodi ya ule wa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ambaye kwa sasa anaonekana atakuwa cha mtoto.

UMRI MIAKA 19 TU LAKINI…
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya kuaminika kwenye duru za habari za mastaa Bongo, tayari Gigy mwenye umri wa miaka 19, amemuwashia taa Wema (27) ambaye kwa ustaa wake wa miaka kumi tangu alipotwaa Taji la Miss Tanzania 2006/07, anadaiwa ‘kuyeya’ na wanaume zaidi ya kumi hadi sasa.

Baadhi ya wanaume waliowahi kuripotiwa kutoka na Wema ni pamoja na wasanii Herry Samir ‘Mr Blue’, Khaleed Mohamed ‘TID’, marehemu Steven Kanumba, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, CK (kigogo), Nagari Kombo, Louis Mnana wa Namibia na Idris Sultan.

Ilidaiwa kwamba, hadi sasa, Gigy yeye anakaribia idadi hiyo ya Wema huku akiwa na ustaa wa miezi kadhaa tu hivyo mashabiki wake hawapati picha atakapotimiza miaka kumi (kama Wema) atakuwa na msururu mrefu kiasi gani!

GIGY ATAHADHARISHWA
“Huyu Gigy ana hali ya hatari maana anaparamia tu mastaa. Kuna watu walikuwa wanamsema Madam (Wema) lakini sasa Gigy ni moto wa kuotea mbali.

“Ana umri mdogo lakini ana mambo makubwa balaa! Bora hata Wema kwa sababu anaweza kujitetea kwa kigezo cha umri na muda alionao kwenye ustaa lakini Gigy bado kabisa kwa kila jambo, si ustaa wala umri.
“Tunamuombea asiingie pabaya maana si unajua tena ulimwengu wa mastaa una majanga mengi!? Anachotakiwa kufanya Gigy ni kujipima kisha kupunguza kasi aliyonayo la sivyo atajikuta kwenye majanga,” alisema mrembo Zuri, mmoja wa mashabiki wa Gigy.

GIGY NA HEMED PHD
Ilidaiwa kwamba, kabla ya ustaa, ukiacha wasanii wasiokuwa na majina makubwa, Gigy alitoka kimapenzi na staa wa muziki na sinema za Kibongo, Hemed Suleiman ‘PHD’, jambo ambalo hivi karibuni Gigy alilikiri katika mahojiano maalum mbele ya Kamera za GlobalTV Online.

Kwa upande wake, Hemed hakupatikana hewani kujibu skendo hiyo ambayo mara kadhaa Gigy amekuwa akiisema kwenye vyombo vya habari.

GIGY NA RICH MAVOKO
Mbali na Hemed, pia Gigy alikiri kutoka kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Richard Lusinde ‘Rich Mavoko’ ambaye aliingia kwenye bifu zito na Hemed, kisa kikidaiwa ni penzi la mwanadada huyo.

Akizungumzia ishu hiyo, Rich Mavoko alidai kuwa hakumbuki kama aliwahi kukutana na Gigy na kwamba kuhusu bifu na Hemed kwa sababu ya mrembo huyo, basi aulizwe Hemed.

GIGY NA KIBA
Mwanzoni mwa mwaka huu, Gigy alidaiwa ‘kuchepuka’ kwa siri na staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ mara tu baada ya kumaliza kufanya shoo kwenye Ukumbi wa Maisha Basement jijini Dar.

Hata hivyo, Gigy alipobanwa juu ya uhusiano wake na Kiba alidai jamaa huyo alimkataza kuzungumzia penzi lao ingawa mrembo huyo alikuwa ameshaachia picha zao za kimahaba wakijiachia.

Hata hivyo, ishu hiyo ilivuja siku chache baada ya Gigy kumlalamikia aliyekuwa mpenzi wa Kiba, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kuwa alimuibia mpenzi wake huyo.

WENGINE HAWA HAPA
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, mastaa wengine waliotajwa kwenye orodha hiyo ya Gigy ni pamoja na wa Bongo Fleva, Emmanuel  Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Seif Shaban ‘Matonya’ na Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ ambaye picha zake za kimahaba na mrembo huyo ziliibua gumzo kubwa.

GARDNER VIPI?
Mbali na wasanii hao, mastaa wengine wanaotajwa kwenye mtungo wa Gigy ni pamoja na Mtangazaji wa Clouds FM, Gardner G. Habash ‘Captain’ ambaye kwenye picha zao mtandaoni wakiwa kimahaba, mrembo huyo alimwita Captain ‘mzee mwenzake’ huku akiapa kuwa yupo tayari kujaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mke wa mtangazaji huyo, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’.

GIGY NA IDRIS
Hivi karibuni, Gigy alioga matusi kutoka kwa lile kundi korofi la mtandaoni linalojiita Team Wema baada ya kuvuja kwa picha zake za kimahaba akiwa na Mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan ambaye ni mpenzi wa Wema Sepetu huku kukiwa na madai kwamba ‘walichepuka’.

GIGY NA TEKNO
Makabrasha ya gazeti hili yanaonesha kwamba, ukiwaweka pembeni mastaa hao wa Kibongo, Gigy aliwahi kukiri kulala hotelini na Mwanamuziki wa Nigeria, Tekno Milles alipotua nchini mapema mwaka huu kwa ajili ya shoo.

AMANI LAMBANA GIGY
Amani lilipombana kuhusu kuwa na msururu wa mastaa, Gigy alifunguka: “Wapenzi wangu wanajulikana na wao ndiyo wananishobokea kwa sababu nalipa ila kwa sasa mimi nina mtu wangu ambaye tunapendana kwa dhati.”

GIGY NI NANI?
Gigy ni video queen, mwimbaji na modo wa kujitegemea ambaye mbali na kazi ya sanaa, amepata umaarufu kupitia picha zake za utupu kwenye mitandao ya kijamii.

Video ambazo amewahi kuuza sura ni pamoja na Ujuzi (ya msanii Climax), Just Wanna Love You (ya Navy Kenzo), Siachani Nawe (ya Baraka De Prince), Nasema Nawe (ya Diamond Platnumz), Kipi Sijasikia (ya Profesa Jay) na Shika Adabu Yako (ya Nay wa Mitego).

Gigy aliyetamba na ngoma yake ya Majojorijo kabla ya kuachia Wimbo wa Supu hivi karibuni, amewahi kufanya kazi kwenye Kituo cha Runinga cha EATV katika Kipindi cha Friday night live.

Kiba, Diamond kimenuka tena...

Kiba, Diamond Kimenuka Hatari!

Stori: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Kimenuka! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mafahari wawili wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kudaiwa kutupiana vijembe vya kufa mtu baada ya kuwepo kwa madai ya Kiba kuhujumiwa.

Kwa mujibu wa chanzo makini, ili kuweka hujuma ya kibiashara, hivi karibuni, pamoja na kukanusha mara kadhaa kutokuwa na tatizo na Kiba, Diamond alidaiwa ‘kutengeneza’ kwa makusudi penzi la mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe na msanii wa Wasafi Classic Baby (WCB), Rajabu Abdulhan ‘Harmonize’ kisha kuvujisha video ya uhusiano huo mpya siku ambayo Kiba alikuwa akiuachia wimbo wake mpya wa Aje (Jumamosi iliyopita), lengo likiwa kuhamisha upepo mashabiki kutoka kwenye wimbo mpya na kujali mapenzi ya wawili hao.

“Ni hujuma ya kibiashara, Diamond na uongozi wake wameamua kumfanyia Kiba ili wimbo wake ukose kiki kwa watu,” kilidai chanzo chetu.

VIJEMBE VYATAWALA

Hata hivyo, kwa mujibu wa mmoja wa mameneja wa Kiba ambaye hakupenda jina lichorwe gazetini, amemtupia vijembe Diamond kwa kudai licha ya hujuma hizo lakini hawawezi kumgusa Kiba.

“Wanajisumbua, kizuri huwa kinajiuza chenyewe na huwezi kuzuia mafuriko kwa mikono. Wameingiza kiki zao lakini msimu huu hazifui dafu. Wimbo (Aje) umepokelewa vizuri na una mafanikio makubwa hadi sasa.

AZUNGUMZIA MKATABA

“Kuonesha kwamba Kiba amekubalika, ndani ya muda mfupi baada ya wimbo huo kuruka hewani, amelamba mkataba na kampuni ya kimataifa ya Sonny Music. Sasa hapo ndipo utakapoona Ngoma ya Kiba imekubalika kiasi gani, hawamuwezi huyu,” alisema meneja huyo.

KEJELI SASA!

Kama hiyo haitoshi, meneja huyo alizidi kutupa vijembe kwa Diamond kwa kueleza kuwa Kiba ni mkongwe hivyo kamwe hawezi kulingana naye kimuziki.

“Diamond hamuwezi Kiba, ameanza kuimba wakati Diamond bado hajawa msanii. Ameshafanya mengi kwenye huu muziki kuliko huyo Diamond, unakumbuka dili la One 8, Kiba aliungana na mastaa wakubwa katika project iliyokuwa chini ya msanii mkali duniani, R-Kelly (Robert Sylvester Kelly), Watanzania wanajua,” alisema meneja huyo.

KIBA HUYU HAPA

Alipoulizwa Kiba kuhusiana na vijembe na kejeli hizo anazodaiwa kuzitupa kwa mpinzani wake (Diamond), alisema ishu hiyo isiitwe vijembe badala yake ieleweke kwamba ndiyo ukweli.

“Siyo vijembe wala majungu. Huo uliosikia ndiyo ukweli wenyewe,” alisema Kiba.

TEAM DIAMOND WAJIBU MAPIGO

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, wafuasi wa Diamond waliojipa jina la Team Diamond walicharuka kusikia msanii wao amehusishwa na hujuma za ‘kumuua’ Kiba kibiashara.

“Hana lolote huyo, Diamond ameshafanya makubwa sana ndani ya muda mfupi kumzidi yeye ndiyo maana anatapatapa kwa sababu nani asiyejua kuwa Diamond yupo fasta katika kuona fursa kuliko Kiba?

“Wolper na Harmonize wapo penzini kwa matakwa yao na si kwa kumuua Kiba, hana jipya,” aliandika mmoja wa wafuasi wa Diamond kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram.

DIAMOND ANASEMAJE?

Jitihada za kumpata Diamond ili azungumzie suala hilo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kutopatikana hewani hadi tunakwenda mitamboni lakini meneja wake, Babu Tale alipoulizwa kuhusu suala hilo, alicharuka:

Risasi Jumamosi: Tale tuambie, hivi kuna ukweli wowote kwamba Diamond na timu yako mlipanga kumzima Kiba alipokuwa anatambulisha ngoma yake mpya kwa kutupia video inayoonesha uhusiano wa Wolper na Harmonize?

Tale: “Siyo kweli. Hilo swali ni la kipuuzi. Sikiliza, ngoja nikuunganishe na bosi wako ili asikie unavyoniuliza. Nakata halafu nakupigia.

Hata hivyo, Babu Tale hakufanya hivyo na alipopigiwa tena, simu yake haikupatikana.

WOLPER AFUNGUKA

Gazeti hili halikuishia hapo, lilimtafuta Wolper ili kujua kama ni kweli ametumika kumfifisha Kiba kimuziki ambapo alisema si kweli kwani penzi lake na Harmonize limetoka katika mioyo yao.

“Hakuna kitu kama hicho. Sisi tumependana wenyewe wala hatujashinikizwa na mtu yeyote kuvujisha penzi letu eti ili kumfanya fulani afifie! Kama imetokea limevuja wakati ambao huyo Kiba naye ametoa wimbo itakuwa tu imetokea lakini si kwamba tumedhamiria,” alisema Wolper huku simu ya Harmonize ikiita bila kupokelewa.

Ugomvi wa Diamond na Kiba ni wa muda mrefu ambapo huwa na msimu kwani kuna wakati unachachama na kupooza kwa mda fulani.

Jini Husnat, sehemu ya pili.

RIWAYA JINI HUSNAT
MTUNZI: ZUBERI MAVUGO
SEHEMU YA PILI

ilipofika jioni wakati anajiandaa kuondoka ghafla mlango ukafunguliwa na HUSNAT akaingia na tabasamu pana usoni uzuri wake ulikuwa mara mbili ya mwanzo bumbuwazi likauvaa uso wa VERGA akutegemea kama angekuja kweli mbona secretary wake ajampgia simu? alijawa na khofu ulochanganyikana na woga ilikuwa lazima aogope alikuwa kavaa gauni jekundu refu lililo mkaa vyema.akaenda kuketi kwenye viti vya wageni na kumpa mkono VERGA........

Mbona SECRETARY wake MOURENE ajampigia simu kumwambia juu ya mtu kumuitaji? au akumwona? au amemdhuru? au naye ameogopa? maswali hayo mfululizo yakakishambulia kichwa chake! akakiri kutoyajua majibu yake akagutuka baada ya kuuona mkono wa JINI yule
"vipi sweet?" sauti tamu imtoaye nyoka pangoni ilipenya katikati ya ngoma ya masikio yake ikawa burudani tosha ndani ya mfumo mzima wa masikio! lakin burudani hiyo katu aikuwepo katika ubongo wake ubongo wake ulikuwa katika tafakari zito tafakari lililomezwa na woga.JOHN VERGAN alitaitika! alikuwa akitetemeka na kusogea nyuma mara ghafla kiti kikadondoka!
"unaogopa nini sweet au aunipendi?" HUSNA kwa mara nyingine tena akauliza! VERGAN akujibu! akabaki kimya
"VERGA TAMBUA NA KUPENDA! NA UKIKUBALI KUWA NA MIMI NITAKUTAJIRISHA UTAMILIKI MALI NYINGI ZAIDI YA HIZI!,MAVIWANDA,MAKAMPUNI,UTATEMBEA DUNIA NZIMA UNAVYOTAKA UTAPOKEA ZABUNI MPAKA MWENYEWE UTAZIRINGIA LAKINI UKINI KATAA NTAKUFILISI UTARUDI KIJIJINI MASIKINI MTAOMBA HADI VYAKULA NA UTAISHI MAISHA YA MATESO KATIKA DUNIA HII UTAKUWA UKIZARAULIWA NA KILA MTU CHAGUA MOJA.....KUMBUKA USINIKATAE KISA MIMI NI JINI! TAMBUA HATA SISI MAJINI TUNA MIOYO YA KUPENDA KWA DHATI ZAIDI YENU NYINYI BINADAMU HIVYO MOYO WANGU UPO KWAKO WEWE VERGA AU UJAVUTIWA NA MIMI?" aliuliza HUSNA huku akiwa anatembea tembea ofisini mule
"hapana! hapan...." ghafla kitasa cha mlangoni kikawa kina tingishika kuonesha mlango unafunguliwa kutoka nje "JINI HUSNAT AKATOWEKA apo apo"
"bosi unaongea na nani? bosi kuna nini? bosi mbona chini umefanya nini?" MOURINE alimuuliza maswali Mfululizo VERGA aliyekuwa kadondokea kwenye pembe ya nyumba
"ulivyo ingia ujamwona mtu?"
"mtu? mtu gani bosi mbona sikuelewi?"
"HUSNA! ujamwona HUSNAT?"
"Husna ndo nani bosi?"
kabla VERGAN ajajibu swali lile HUSNA akatokea na kumnyooshea VERGAN kidole mdomoni ishara ya kunyamaza.
"amna kitu MOURINE kaendelee na kazI"

"Amna kitu MOURINE kaendelee na kazi!"
alijibu VERGAN huku akinyanyuka na kujifuta futa vumbi HUSNAT ALISHATOWEKA!
"Bosi kuna wale watu wa idara ya mapato wanasema watakuja kesho ivyo uandae risiti zote"
"sa...w ni.meku..elewa" VERGAN alijibu kwa kubabaika secretary wake akaondoka VERGA akarud kwenye kiti chake na kukaa kitu "AKIKUKALIKA!" alinyanyuka na kuchukua koti! lake la suti lililokuwa nyuma ya kiti chake na kulivaa.akachukua simu na kumpigia MOURINE
"Namuitaji ZUBER"
"Sawa bosi"
baada ya muda ZUBER akaingia,
"sasa wewe kijana kaa hapa ofisini mimi naenda kupumzika kidogo"
"sawa bosi"
JOHN VERGAN akachukua brufcase yake na kuondoka!,aliitaji kupumzika aliisi kichwa kinamuuma,katu akujua balaa alilokuwa akilifata mbele yake

ZUBER alitafuta ma file na kuendelea kuyajaza taratibu! akujua kinachoendelea yeye alikuwa na yake kichwani katika kudhihirisha ule usemi umdhaniaye ndiye kumbe siye,au rafik yako ndiyo hadui yako,ZUBER alikuwa ni chui kwenye ngozi ya VERGAN ama kweli usilo lijua ni sawa na usiku wa kiza.

na kwa upande wa MOURINE secretary wa VERGAN kiti akikukalika! alijua bosi wake ana matatizo tu! japo hakuwai kumwambia kuwa anampenda ila moyoni mwake alikiri kumpenda sana bosi wake yule! hapa kuna kitu na lazima nifanye kitu kumsaidia bosi wangu wakati akiwa anawaza hayo ghafla arufu kali ya manukato ikaanza kusikika,upepo mkali ukaanza kuvuma! vumbi lililotengeneza kimbunga cha wastani kikaanza kuingia ndani na kupeperusha ma file yale pale mezani,makabati yakaanza kujifunga na kujifungua yenyewe na mara mtoto mzuri mrefu alovaa nguo ndefu akatokea! katikat ya chumba kile MOURINE akataka kukimbia akashindwa,akataka kupiga kelele pia akashindwa akabaki na butwaa "mimi naitwa "ZAIDATU BINT ROUJAT" ukoo wa kifalme wa kijini nimekuja kwa ajili ya msaada kwako.ila lazima ufe" kabla MOURINE ajafanya kitu JINI ZAIDATU akamvamia na kumnyonya damu yake.

******

JINI ZAIDATU baada ya kuakikisha amemuangamiza secretary yule MOURINE kwa kumfonza damu yake yote akaa chia ukelele mkubwa! kisha akatoweka! mara ghafla MOURINE akazinduka ilikuwa kama kazinduka toka usingizini! ila MOURINE huyu alikuwa tofauti na wa mwanzo! macho yake yalingaa! meno yalichongoka mawili! ila ghafla vyote vikatoweka akabaki MOURINE wa mwanzo! ZAIDATU alikuwa kaingia katika mwili wa MOURINE kwa kazi maalumu! ni kazi gani? aliijua moyoni mwake.aliendelea kufanya kazi zake kama kawaida.machoni alionekana ni MOURINE ila kumbe alikuwa ni jini hatari ilikuwa ni PATASHIKA.

Moyoni mwa ZUBER wazo lililotawala kichwa chake ni kuakikisha mali zote za VERGAN zinakuwa chini yake kwa namna gani? ilo alikumsumbua akakwa pua simu ilokuwa pale mezani na kupiga namba kadhaa akaweka mkonga wa simu yake maskioni "MOURINE nakwomba uniunganishe na PITER"
"sawa bosi" MOURINE aliitikia.na kuwaunganisha wakaongea machache.

dakika chache zilizofatia PITER au mwanasheria mkuu wa compuny ile alikuw mbele ya bosi wake yule. "nachotaka kuongea na wewe ni siri kukiwa na makubaliano au hata kama kusipokuwa na makubaliano!" ZUBERI alifungua kikao kile kwa onyo kali.
"na kama siri hii ikivuja sitokuwa na kingine zaidi ya kukuua!"
"what?" PITER aliamaki
"ndiyo! ni dili litakalo badilisha maisha yetu tutakuwa matajiri wakubwa kama bosi VERGA"
"SAWA nipo tayari weka kazi mezani!" PITER Alikubaliana na wazo la ZUBER na kuwa tayari kusikia dili lenyewe
"naitaji tutaifishe compuny hii iwe chini yetu! mimi na faida tugawane amsini kwa hamsini"
"unasema?"
"ndiyo naitaji compuny hii iwe chini yetu"
"sijakuelewa ZUBER ni vipi tutafanikisha ili?"
"swali zuri PITER wewe ni mwanasheria wa compuny una nyaraka hati zote muhimu ni kitendo cha kuzibadilisha tu"
"tatizo itakuwa nisahii yake"
"atatekwa na kulazimishwa kuweka sahii baada ya hapo tutamuua"
"sawa ZUBER nimekuelewa niachie nianze kazi..

*******
JOHN VERGAN alifika nyumbani kwake na mlinzi akafungua geti VERGAN akaingiza gari taratibu.mlinzi alimsalimia lakini VERGAN akuitikia.kichwa kilikuwa kikiwaka moto akaenda mpaka chumbani kwake na kujitupa mara ghafla akapitiwa na usingizi wakati akiwa yupo usingizini akaota yupo na JINI HUSNA akiwa pembezoni mwa jabali palipokuwa pameota majabali makubwa wakiwa wameegemeana kimapenzi HUSNA akasema:
"dear nna zawadi yako!"
"zawad gan sweet?" VERGAN akaoji akiwa kaushika mkono wa dada yule mrembo
"funga macho yako"
VERGAN akafumba HUSNA akatoa mkufu wa dhahabu na kumvalisha VERGA
"Fungua!"
VERGAN alipofumbua macho yake akuamini akamkumbatia kwa nguvu HUSNA mkufu ule ulikuwa ukimeremeta huku ukiandika jina la VERGAN ulikuwa na picha ya HUSNA na VERGAN wakiwa wamekumbatiana.Baada ya VERGAN kumkumbatia akamwachia ghafla akashangaa kumuona kabadilika kawa na sura mbaya ya kutisha meno yalochongoka pembe pembeni ya vichwa kucha ndefu VERGA akashindwa kuvumilia na kupiga kelele ghafla akazinduka.
"he! kumbe ilikuwa ni ndoto?"
VERGAN alitahayari alishindwa kuzuia mshangao dhahiri katika macho yake.wakati akiwa anashangaa wakati akiwa bado kakaa kitako kitandani.alipocheki pembeni ya kitanda AKAUONA ULE MKUFU! aliruka kitandani na kutaka kukimbia MLANGO UKAJIFUNGA kizaa zaa kikaanza.kelele za msichana akicheka zikasikika.
"VERGAN kwa nini unielewi? kwa nini utaki kunipenda? kwa nini utaki kunizoea? ama uitaji kuwa nami? niambie VERGAN nijue,hata mimi na moyo VERGAN!" ilisikika sauti ikisema na kimya kikafuata mlango ghafla ukafunguka.VERGAN kama mweu akatoka mbio alikimbia hadi getini mlinzi wake ndiye aliyefanikiwa kumzuia
"bosi wangu utaumia! una matatizo gani bosi tell me why?"
"niache! niache! niache KITALU niache!" (come down bosi come down punguza presha,relax,smile ,then tell me why ili niweze kukupa msaada) twende ukaone mkufu twende jini si ndoto ni kweli! VERGAN aliropoka.
***************
VERGAN na mlinzi wake KITALU waliongozana hadi ndani VERGA akiwa na lengo la kumuonesha ule mkufu wa ajabu! mkufu wa ndotoni walipofika AWAKUKUTA KITU!,MKUFU AUKUWEPO,VERGAN akakunguta mashuka lakini bado mkufu aukuonekana.ikabidi kwa maneno kuntu,maneno ya hisia VERGA amsimulie mgambo wake yule!
"bosi wangu! jambo doncho sana ili!,ili ni jini mahaba na kuna ustadh! swadakta maalim! sheghe ni shidaaaa! hana uwezo wa kumwita! kumpumbaza! kumkamata na kumfinyanga hadi aitwe marehemu anaitwa maalim sheghe RAJAB!"
"unaweza kunipeleka saivi kwa maalim?"
"bila shaka kabosi kangu! lakini pale kagetini katakaa kanani?"
"uc of pale ntamtafuta mtu mwingine"
"akah! na mimi si ntakosa ka kazi bos?!"
"hapana we ntakupandisha cheo utaenda katika compuny yang na ela itapanda."
"sawa bosi ngoja nkajiandae ili tukaka angamize ako kajini mahaba!"
ile saa KITALU anageuka tu nyuma akakumbana na mkono dhabiti! mkono imara wa HUSNA! lakin VERGAN akumwona KITALU alihisi kukabwa ghafla akaanza kukooa damu alikuwa akionesha kidole shingoni alipokabwa mara akadondoka chini na kufa hapo hapo.HUSNA akiwa na uso wa hasira akaiangalia kwa chuki maiti ile akairuka na kuweka mikono juu akatoweka.VERGA alichanganyikiwa! kitalu hakuwa mzima na sasa ni marehemu! kivipi? bado lilikuwa swali lisilo na jibu

polisi walikuja na kumchukua VERGA na house garl wake JASMIN na mwili wa marehemu ukapelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi.alama za mikono shingoni zilionekana dhahiri! hivyo madaktari wakaanza kudili nazo.

cha ajabu alama za mikononi za JOHN VERGAN ndo zilizo onekana shingoni mwa MLINZI MACHACHARI KITALU.mshatakiwa namba moja akawa JOHN akawekwa chini ya ulinzi! moyo ulimuuma maswali ya siyo na majibu yakatiririka kichwani kwake.familia yake baba mama zote walikuja kumtembelea wakamtoa khofu kwa kuweka mawakili hatari pesa si ilikwepo.tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi ikafika.baada ya kuamishwa katika mahaka
****************

SERIKALI ikapandisha shaidi namba moja! ambaye alitambulika kama afande MARWA.
MWENDESHA MASHTAKA@"taja majina yako matatu"
SHAIDI NO 1@ "MARWA JAFETY JOHN"
MW/MASHTAK@ "Unaweza kutuambia kilichotokea siku ya tukio?"
SHAID NO 1 "Yap nilikuwa kituoni siku hiyo mara simu ikaita kupokea ni msichana aliyekuwa akilia alidai bosi wake alikuwa akimnyonga mlinzi wake ndipo nilipochukua afande wengine mpaka eneo la tukio tulipofika tulimkuta mtuhumiwa kashafanya mauaji ndo tukawaweka yeye na house garl chin ya ulinzi"

maelezo haya ya AFANDE marwa yalimshtua kila mtu akiwepo JOHN VERGAN ambaye yeye ndiyo aliyepiga simu polisi iweje aambiwe ni mfanyakazi wake? pia mawakili wake walitazamana kwa kutoamini wakisikiacho kesi kwa upande wao ilizidi kuwa ngumu na kwa upande wa house gar yule alishangaa kuambiwa eti alipiga simu wakati bosi wake ndo alipiga ilikuwaje? kuna nin? ilikuwa ni mkanganyiko katika mioyo yao katu awakujua kuwa:

wakati JOHN VERGAN anapiga simu kituoni sauti yake iliishia mule ndani lakin katika masikio ya afande MARWA ilisikika sauti ya binti akiongea kwa jazba,woga,huyu si mwingine ni JINI HUSNAT aliyeyameza maneno ya VERGAN na kuongea kama JASMIN.ndivyo ilivyokuwa.

MW/MASHTAKA "mshtakiwa una swali lolote kwa shaidi no 1"
VERGAN "ndyo mh! afande marwa mimi ndo nlikupigia simu iweje useme ni JASMINI kwa nini lakin inakuwa hivi?"
baada ya kuuliza swali VERGAN akaanza kulaumu ikabidi akatishwe na nafas kurudi upande wa mawakili